Na PETER FABIAN-MWANZA
JANGA jingine. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kutokea   ajali nyingine ya Kivuko Ziwa Victoria wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza.
Kivuko hicho kilipinduka jana baada ya kudaiwa  kilikuwa kimebeba abiria wengi kuliko uwezo wake na kusababisha kuelemea upande mmoja.
Hiyo inakuwa ni ajali kubwa ya pili kutokea ndani ya Ziwa Victoria baada ya miaka 22 wakati meli ya MV Bukoba ilipozama na  watu zaidi ya 1000 walifariki dunia.
Taarifa kutoka wilayani Ukerewe zilieleza kwamba kivuko hicho kilikuwa kinatoka katika kisiwa  cha Ukerewe eneo la Bugorola   kwenda Kisiwa cha Ukara.
Hata hivyo kivuko hicho kikiwa kimebakiza kilometa chache kufika Kisiwa cha Ukara, kilipinduka na kuelea   karibu na daraja la Bwisha.
MTANZANIA ilielezwa kwamba meli hiyo ilianza safari  kutoka Bugorola saa 6.00 mchana kwenda  Bwisha, Ukara.
Inadaiwa   ilikuwa na  zaidi ya abiria 350  kuliko uwezo wake ikizingatiwa  kina uwezo wa kubeba tani 25 ikiwa ni abiria 100 na magari matatu kwa wakati mmoja.
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.