25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

JAMHURI YAWATILIA SHAKA MAWAKILI WA AKINA MBOWE

Na KULWA MZEE

DAR ES SALAAM

UPANDE wa Jamhuri umetilia shaka utayari wa mawakili wa utetezi katika kesi inayowakabili vigogo tisa wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wa kuhakikisha shauri hilo linasonga mbele kwa usikilizwaji.

Hoja hiyo iliwasilishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu  wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri, wakati shauri hilo lilipokwama kuanza usikilizwaji wa awali.

Kesi hiyo ilitakiwa kuanza usikilizwaji wa awali lakini haikuwezekana kwa sababu Wakili Peter Kibatala, alikuwa Mahakama Kuu na Wakili Jeremiah Mtabesya alikuwa Mahakama ya Mtwara.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai upande wa Jamhuri wanatilia shaka utayari wa mawakili wa utetezi wa kuhakikisha shauri hilo kinasonga mbele.

“Mawakili hawa wa utetezi hawaonyeshi utayari wa kuendelea na kesi, tunatilia shaka, tutaongea wenyewe wakiwepo mahakamani, tunafahamu wako wawili lakini mmoja akiwa na udhuru na mwingine pia, tuhakikishe kutokuwepo mmoja kusiathiri kalenda ya mahakama,” alisema Faraja na kutaka mshtakiwa Esther Matiko kueleza dharura iliyomfanya asihudhurie mahakamani wiki iliyopita.

Matiko alijieleza kwamba binti yake aliumwa shuleni Kenya hivyo alilazimika kwenda kwa ajili ya kumsaidia kupata matibabu.

Hakimu Mashauri alimwonya Matiko kwamba asirudie tena kumtuma mdhamini kwa kumwambia kapata dharura bila kueleza dharura yenyewe.

Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 13, mwaka huu  kwa ajili ya kuanza usikilizwaji wa awali.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi alidai kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya usikilizwaji wa awali na kwamba kwa upande wao wako tayari ila mshtakiwa wa tano Matiko hakuwapo.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee,   Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya na Mbunge wa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles