25.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Jaji Mtungi avitaka vyama vya Siasa kukuza ushiriki wa wananwake katika maamuizi

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa nchini kukuza ushiriki kwa wanawake katika ngazi za maamuzi ilikuweza kukuza Demokrasia nchini.

Akizungumza leo Aprili 25, 2023 katika warsha ya kupitia Mapitio ya uchambuzi wa mapengo ya kijinsia katika Nyaraka za Kisera za vyama vya siasa jijini Dar es Salaam, Jaji Mutungi amesema vyama vya siasa vinamchango mkubwa katika ngazi ya uongozi nakukuza haki ya ushiriki katika fursa mbalimbali zilizopo kwenye vyama hivyo.

“Nchi ya Tanzania inajumla vya vyama 19 vinavyoshiriki katika uchaguzi lakini kwenye majimbo mengi ya vyama kumekuwa idadi ndogo ya ushiriki wa kijinsia katika uchaguzi na uongozi,” amesema Jaji Mtungi.

Amesema kuwa ni vyema vyama vya siasa kuzingatia usawa kijinsia katika vyama hasa katika ngazi za uongozi.

Amesema ni muhimu vyama vya siasa kuyafanyia kazi mapendekezo yanayotokana na kukuza ushiriki katika uongozi hasa mchakato wa kisiasa kwa wanawake.

“Ni muhimu kuyafanyia kazi mapendekezo haya yaliyopo katika ripoti hii kuhusiana kukuza ushiriki katika siasa hasa kwa wanawake,’ amesema Jaji Mtungi.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia nchini, Profesa Ibrahim Lipumba amesema ushiriki wa wanawake katika masuala ya siasa na uongozi upo chini sawa na asilimia 51 kwa wanawake waliofikisha umri wa miaka 18.

Amesema idadi hiyo ni ndogo ukilinganishwa na nchi ya Rwanda ambapo ushiriki katika uongozi ni asilimia 61 hasa kwa ngazi ya ubunge.

“Tunahitaji uwakilishi mkubwa kwa wakina mama hasa kwenye mifumo vyama vya siasa katika nchi za Bara la Afrika zinazongoza kwa ushiriki wa wanawake katika uongozi ni Rwanda, Mauritius na Botswana,” amesema Profesa Lipumba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles