26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

HURRICANE HARVEY: KUMBUKUMBU YANGU

Na, MWANDISHI WETU


BAADA ya kuharibika sana, akili ya binadamu itarudi kwenye kazi yake ya kawaida na kuweka janga hilo kama sehemu ya historia kwa miaka ijayo.

Hii ina maana kuwa wataalamu na wabobezi wa historia wataweka hii kwenye kumbukumbu zao ilhali wenyeji watakuwa na kitu cha kuzungumza juu ya kumbukumbu hiyo ya milele.

Lakini pia inaturuhusu na kutupa nafasi ya kufikiri zaidi juu ya maisha na ni nini kinakuja katika taswira tofauti.

Bado wanasubiri  wakiwa na matumaini kuwa hiki kitakuja kama ilivyo kuwa Ike, Rita, Katrina na sasa Harvey, utajua namna gani tunavyohisi katika kuishi kwenye vimbunga vyote hivi tukiwa sehemu ya ushuhuda wa maisha na maelezo yote yanayosisimua huku kila mmoja akitafuta namna yake ya kuyakabili.

Ni wazi kuwa hasara haiwezi kufidiwa kwani tunatambua kuwa watu walihamishwa, walipoteza mali, vifo vilitokea, magonjwa, machafuko na kila aina ya hadithi zisizojulikana kama unavyoweza kuziita.

Miongoni mwa mambo mengine mengi, maafa haya yamekuwa yakiwaleta watu pamoja ambapo majirani huzunguka na kuzungumza pamoja, watu watatoa ushuhuda huu huku familia zikisema na kuwasalimu, chakula hukosekana kwenye masoko, mwanga huondoka, matumizi ya pombe huongezeka maradufu, sala kwenda mahala pengine bila kusahau barabara kufunikwa na maji.

Lakini pia nyumba zitazingirwa na kujaa maji, watu watashindwa kuonana hasa rangi ya ngozi zao au rangi yao halisi huku usiku na siku zikiwa ndefu zaidi kuliko kawaida.

Mwanadamu ataondolewa kutoka kwenye mzunguko wake wa kawaida kwenda kwenye ule usiotabirika ambapo huko hakuna mtu ambaye anaweza kuishi maisha yake ya kawaida kama ilivyokuwa awali, ambapo aina hiyo ya maisha itakuwa imefungwa kama mpira wa miguu usiokuwa na upepo ndani yake.

Pale ninapomeza mishipa yangu ili kupata maono sahihi ya kile ninachokiona nikiwa nimeketi katika kona ya Crib nikiangalia nje ya dirisha na mbwa wangu Champ akiwa ameketi katikati ya miguu yangu ambaye amelala kwa sauti bila ya kuwapo na chochote cha kuogopesha kuhusu kulinda usalama wangu na wa kampuni kama AmbAvyo amekuwa akifanya siku zote.

Nashuhudia maji yenye ukubwa wa futi tano kwenda juu ya usawa wa ardhi nje na ndani ya mifereji ya maji, hewani hakuna ndege, gari na kuna utulivu kama mji wa roho ambao umenisukuma mimi kurejea Hurricane Katrina.

Siku za nyuma ambazo nilihamia katika Mji wa Dallas kwa wiki mbili ambao ni umbali wa saa nne kutoka Mji wa Houstone nikisubiri mji wangu uweze kurejea kwenye hali yake ya kawaida, nikiwa njiani kuelekea Dallas ilikuwa ni ngumu kwangu kukata tamaa baada ya kuona familia pamoja na wapendwa wao wakipambana kuelekea mahala kusikojulikana kwa ajili ya usalama wao.

Ilikuwa ni hali ngumu na mbaya kuweza kuivumilia japo nilibaki nikijiuliza swali moja tu kubwa ambalo ni Je, maisha ni nini?

Jumapili ya saa 12:53 jioni nimekuwa nyumbani tangu ijumaa asubuhi na niliambiwa kuwa tutaendelea na maisha ya kawaida ifikapo Ijumaa asubuhi au baada ya siku saba kadri itakavyowezekana.

Hata hivyo naangalia nje na kuona mvua nzito na kubwa ya mawe ikinyesha huku mawe hayo yakigonga mlango na kufanya nyumba  itetemeke.

Mbali na dhoruba hilo la mawe pia mvua hii iliambatana na mawimbi makubwa, ambapo kwa hali hiyo ni wazi kuwa hakuna namna nyingine zaidi ya kutazama na kusikiliza habari mbalimbali zinazoendelea kurushwa kupitia vyombo vya habari huku nikila asali na kujiambia kuwa kama Mungu ameweza kuumba nyumba hii basi ataweza kuilinda pamoja na watu walioko ndani yake.

Haikuwa inaruhusu mtu kwenda kufanya kazi na kupata pesa kama inavyotakiwa kila siku kwa ajili ya kupigania uzima, lakini ilikuwa inahitajika jitihada binafsi kuona kinachotokea karibu yako na ulimwenguni kwa ujumla.

Mungu anasema na sisi na amekuwa akitumia ishara mbalimbali kila siku na kila wakati, lakini sisi tuko bize sana kugawanya ujumbe wa kweli na kujifunza kwa wenye nguvu na kushindwa kuelewa kuwa sisi wenyewe tumekuwa tukichukua vitu kwa nafasi.

Dunia inaweza kuwa na inapaswa kuwa mahali bora zaidi pakuishi kuliko sasa na hii itawezekana ikiwa tutafanya mambo bora na kumshukuru Mungu mmoja na aliyeweza sana.

Nimejaribu kuwashirikisha na ninyi kumbukumbu yangu hii ndogo huku nikitumia wakati huu kuinua maisha yangu, naamini kuwa kumbukumbu hii inaweza kuwa ndogo kuliko tutakayoyapitia lakini ukweli nikwamba Mungu ana udhibithi na yote haya yatakuwa yanapatikana na kudhibitiwa.

Hata hivyo nina hakika kwamba ujumbe wangu utafika ambapo unatakiwa na tafadhali uwe mgeni wangu na tuombe wote kwa ajili ya dunia na Texas.

Taifa la Marekani likiwamo Jimbo la Texas limekuwa likikabiliwa na changamoto ya kimbunga mara kwa mara jambo ambalo limekuwa likisababisha familia nyingi zaidi kutafuta makazi sehemu nyingine.

Hii inatokana kwamba aina hiyo ya vimbunga vikali vimekuwa vikishindwa kudhibitika na mamlaka husika na hivyo kulazimika kutoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo tajwa kuweza kuhama kabla ya kukumbwa na madhila hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles