21.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 26, 2024

Contact us: [email protected]

Heinken yanunua kampuni za Distell na Namibia Breweries

Na Mwandishi wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya Heinken imetangaza kununua kampuni ya Distell Group Holdings(‘Distell’) na ile ya Namibia Breweries (NBL) ambapo ununuzi huo unafikia zaidi ya Euro Bilioni 1 katika mapato halisi.

Pia, ununuzi huo umefikia Euro milioni 150 katika faida ya uendeshaji wa nyayo zao za Afrika ambapo utachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam Mei 22, 2024 na Meneja Mkazi wa Kampuni ya Heinken, Obabiya Fagade, ambapo amesema wamepewa nafasi pekee kufikia hadhira pana zaidi kutokana na upanuzi wa kazi zao kutokana na ununuzi wa kampuni hizo.

”Kampuni inayoongoza duniani ya kutengeneza vinywaji Heineken inatarajia kuzindua rasmi jalada na chapa ya kampuni mpya ya aina mbalimbali itazinduliwa Mei 25 mwaka huu, kufuatia kukamilika kwa ununuzi wa kampuni hizo mbili za Distell na NBL,” amesema

Amesema Heineken kwa sasa inapatikana katika masoko 114 na kuuzwa katika zaidi ya masoko 180 na iko tayari kuwa kiongozi wa soko katika tasnia ya vnywaji nchini Tanzania.

Kwa upande wake Mkuu wa Biashara na Masoko ya Kampuni hiyo, Lilian Pascal, amesema tangu mwaka 1,864 wamekuwa wakisambaza bidhaa yao ya heineken na kufika katika mataifa mbalimbali.

Amesema katika kuwekeza nchini Tanzania Kampuni imeendelea kuamini sera za uwekezaji wa Tanzania na uwepo wa mazingira salama chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza chapa yao.

”Ushindani upo katika biashara yoyote, sisi tunatoa bidhaa yetu iliyobora na iliyokidhi vigezo na ndio maana hadi leo tupo katika soko muda mrefu,” amesema.

Aidha, amesema mgeni rasmi anatarajia kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mpango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo na viongozi wa tasnia mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles