KISPOTI: Hivi sasa umesimamishwa kucheza michezo mitano iliyosalia katika klabu ya Simba ili kukamilisha msimu wa 2015/16 Ligi Kuu,unalizungumziaje hilo?
Kessy: Lolote linaweza kutokea kwenye soka, kuna usemi wa kiswahili unaosema akufukuzae akwambia toka, hivyo kusimwamishwa kwangu kunaonyesha wazo mimi si mchezaji wa Simba tena, kwani pindi adhabu yangu itakapomalizika na mkataba wangu utakuwa umefika mwisho.Nashukuru wamenipa muda wa kufanya mambo yangu mengine.
KISPOTI: Ungependa kuwaeleza nini viongozi wa Simba?
Kessy:Nawashukuru kwa muda wote nilioishi nao, hivi visa,vituko na kutofautiana hakukuanza leo, ila sikuwahi  kuonyesha ishara yoyote iliyoashiria kuwa nimechoka kufanya kazi nao, sina kinyongo nao nikiamini malipo ni hapa hapa duniani.
KISPOTI:Vipi kuhusu kumsamehe mchezaji mwenzako Vicent Angban, ambaye aliamua kukupiga, baada ya kumalizika kwa mchezo wenu na Toto African hivi karibuni.
Kessy: Ukweli bado nafsi yangu haijamsamehe Angban kwa kitendo alichokifanya, tumekutana katika kazi na alinishutumu kwa kitu ambacho sijakifanya naweza kusema kuwa alitumia unyonge wangu kunipiga ipo siku nay eye atakutana na mbabe wake.
KISPOTI: Mgogoro wako na Simba umekuathiri vipi?
Kessy: Nimeathirika kwa kiasi kikubwa, kwani baada ya kutokea ugomvi wa mimi na Angban , taarifa zilifika nyumbani kwetu na wazazi walinilaumu wakidai nimeanza tabia zisizo fahaa, lakini nashukuru meneja wangu Athuman Tippo aliweza kuwaelewesha.
KISPOTI:Mipango yako ijayo kisoka ipo vipi, tayari umeanza kuhusishwa kwenda Yanga?
Kessy: Kwa sasa nipo huru ni mapema kusema naenda wapi, ingawa muelekeo na matamanio ni kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini.