29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Halima Kopwe aomba uwekezaji tasnia ya urembo

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mwakilishi wa Tanzania kwenye shindano la ‘Miss World 2024’, Halima Kopwe ameiomba serikali kuwekeza katika tasnia ya urembo kama inavyofanya kwenye mpira kwani itasaidia kuitangaza nchi lakini pia kuvutia vijana wengi.

Halima ameyasema hayo Machi 13,2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wake kwenye mashindano hayo.

Amesema tasnia ya urembo inahitaji uwekezaji kama kwenye tasnia nyingine ili hata ikitokea mashindano ya kimataifa iweze kuiwakilisha vyema nchi.

“Sisi kama nchi tunakila kitu maana hata nilivyoshiriki haya mashindano ya Miss World sijaona kitu kikubwa ambacho kama nchi hatuwezi kufanya sema wenzetu wamewekeza sana unakuta mtu vazi la ubunifu anavalishwa na mbunifu mkubwa wa nchi husika tofauti na sisi mpaka utafute mwenyewe, mimi naamini serikali ikiwekeza kwenye tasnia hii kama wanavyofanya kwenye mpira tutafika mbali,”amesema.

Amesema ameweza kuiweka nchi kwenye rekodi nzuri baada ya kuingia kwenye kumi bora ya Beuty With a Purpose kupitia kazi yake ya Damu Yangu Kizazi Changu yenye lengo la kumsadia mama na mtoto.

Amesema pamoja na kuingia 10 bora lakini kwenye fainali aliingia 40 bora ambapo ushindi huo kama nchi iliupata mwaka 2005.

Aidha ametoa rai kwa wadau pamoja ya kuwa mradi huo upo chini ya taasisi ya Miss Tanzania bado inahitaji kuendelea kuisaidia jamii yake kama sehemu ya maisha yake ameomba wadau kumsapoti ili apate gari la wagonjwa kwa ajili ya kupeleka gari hilo katika mkoa wa Mtwara.

Naye Mkurugenzi wa ukuzaji na maendeleo ya sanaa Baraza la Taifa la Sanaa (BASATA) ameipongeza kamati ya Miss Tanzania kwa kuweza kumsimamia mrembo huyo hadi kuiletea nchi heshima, hivyo wameahidi kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha tasnia ya urembo inaendelea kuiwakilisha nchi kwenye mataifa mengine.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya The Look, Halima Mhando amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ameitendea haki tasnia ya urembo na sanaa kwani hata mafanikio makubwa yaliyopatikana kupitia uwekezaji mkubwa anaoufanya lakini pia kuitangaza nchi kupitia filamu ya The Royal Tour ambayo imefanya nchi kujulikana kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles