29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Hali za polisi mbaya, DCI Mungulu ashutushwa

Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mngulu

Na Amon Mtega,  Songea

HALI  za askari polisi watatu waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, baada ya kujeruhiwa na bomu lililotengenezwa  kienyeji imeelezwa kuwa ni mbaya.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Issaya Mungulu alisema jopo la madaktari linaendelea kutoa matababu kwa askari hao.

Aliwataja askari ambao hali zao si nzuri kuwa ni  kuwa G7351 PC Ramadhan ,WP 10399 PC Felista wakati  H 3484 PC Respicus ametibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

MKURUGENZI wa upelelezi wa Makosa ya Jina nchini CP  Issaya  Mngulu amethibitisha kuwa Bomu waliotupiwa Askari  polisi wannewaliokuwa wanne  limetengenezwa kienyeji na kwa kitaalam zaidi kuliko mambomu mengine yaliyotengenezwa kienyeji  ambayo  yaliyowahi  kulipuriwa katika maeneo mengine nchini  ambapo hadi sasa hakuna mtu aliyeshikiliwa.

Alisema askari hao walikuwa wakifanya doria katika eneo la Mfaranyaki kuelekea Matalawe, lakini walipofika  mtaa wa Mabatini karibu na nyumba ya kulala wageni ya Maliatabu kata ya Misufini  ghafla walisikia kishindo kizito kikitua mbele yao.

Alisema msako mkali unaendelea ili kubaini watu waliohusika na tukio wanatakiwa mbaroni.

“Ndugu waandishi hawa waliofanya tukio ili tunaamini ni sehemu ya jamii tunayoishi nayo na mtu aliyetengeneza bomi hili ni lazima kuna mtu au watu waliomshuhudia au wanaomjua… kwa maana hakuwa peke yake, tunaomba wananchi watupatie ushirikiano.

“Nimekagua matukio mengi  nchini yanayohusiana na milipuko ya mabomu, lakini tukio la Songea  ni la aina yake.

Bomu linaonekana linakava  ya bati gumu  ambalo linaonyesha limetengenezwa kiufundi zaidi ,”alisema Mngulu.

Wakati huo huo, majeruhi wawili walioumizwa katika tukio hilo, wamesema hali zao zinaendelea vizuri  na tayari wameshafanyiwa upasuaji. Akizungumza na waandishi wa habari wodi  hapo,PC Ramadhan alisema  alifanyiwa upasuaji wa mguu wa kulia na kuondolewa masalia ya  vibati viwili.

Alisema pia amepata michubuko sehemu za mgongoni na tumboni ambako kumetobolewa na kitu chenye ncha kali. Naye WP Felista, alisema   bado anasumbuliwa na mguu wa kulia, ingawa ameanza kupata nafuu. Hata hivyo, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, Dk.Benedicto Ngaiza alisema   hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri.

Alisema WP Felista ameumia zaidi kwenye mguu wa kulia  kutokana na kuvunjika  mifupa mmoja. Tukio la askari hao, lilitokea juzi wakati watu wasiojulikana walipowarushia kitu kinachosadikuwa kuwa bomu na kuwajeruhi vibaya.Hadi jana hali kuna ambaye alikuwa amekamatwa.  Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles