28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

‘HAKUNA UTAFITI SIDIRIA KUSABABISHA SARATANI’

Na VERONICA ROMWALD –DAR ES SALAAM

SERIKALI imewatoa hofu wanawake nchini juu ya uvumi wa kuwapo kwa sidiria zinazodaiwa kupandikizwa majimaji yanayosababisha saratani ya matiti.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mratibu Programu ya Saratani ya Via vya Uzazi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Safina Yuna, alipozungumza na MTANZANIA Jumamosi katika mahojiano maalumu.

Mahojiano hayo yalilenga kujua hatua mbalimbali ambazo Serikali inazichukua kukabili ugonjwa huo ambao unaonekana kusababisha vifo vya wanawake wengi baada ya saratani ya kizazi na ngozi.

Akizungumza Dk. Yuna, alisema hadi sasa hakuna utafiti wowote ambao umewahi kufanyika popote kuthibitisha ukweli juu ya madai hayo.

“Ni dhana potofu, jamii isiwe na hofu, kitaalamu haijagundulika nini hasa kisababishi cha saratani hii lakini kuna (risk factors) tabia

hatarishi ambazo zinatajwa kuwa zinaweza kuwa kichocheo cha kumsababishia mtu kupata saratani ya matiti.

“Kwa mfano wapo ambao wanaweza kupata kwa kurithi yaani ikiwa kuna mtu kwenye familia au ukoo aliwahi kuwa na ugonjwa huo wapo ambao wanaweza kuja kurithi hapo baadaye,” alisema na kuongeza:

“Unywaji pombe, uvutaji sigara na kitendo cha mwanamke kuchelewa kuzaa na kutonyonyesha mtoto huweza kumweka kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu.”

Alisema kwa mujibu wa takwimu kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI), kila mwaka tunapokea wagonjwa wapya 50,000 kati ya hao asilimia 12 huwa wanagundulika kuwa na saratani ya matiti.

“Kati ya asilimia 12 ambao hugundulika asilimia 9.7 hufariki dunia, asilimia 99 ya wanaopata saratani hii ni wanawake, wanaume huwa asilimia moja tu,” alibainisha.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles