25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

GUARDIOLA: KWA MAN CITY HII, SINA MPINZANI

MANCHESTER, ENGLAND


BAADA ya klabu ya Manchester City kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea, kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola, amefunguka na kusema hana mpinzani kutokana na ubora wa kikosi chake.

Kocha huyo anaamini kuwa kikosi chake kinaweza kwenda kucheza nje ya Uwanja wa Etihad na kufanikiwa kupata matokeo mazuri, hivyo anaamini hakuna mpinzani ambaye anaweza kumtisha kwa sasa.

Man City juzi walikuwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na kiungo wake, De Bruyne, alikuwa mchezaji wa pekee ambaye aliwafanya mashabiki wa Chelsea walale na viatu baada ya kichapo hicho.

“Jambo muhimu kwetu lilikuwa kushinda kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na kuondoka na pointi tatu, nataka kuifanya Manchester City kuwa kwenye ubora wa hali ya juu kwenye michuano ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Kwa sasa ninaamini wachezaji wapo pamoja na mimi kutokana na kufuata yale ninayowaelekeza, kila mmoja alikuwa anajua ubora wa Chelsea, lakini tuliweza kuushambuliaji Uwanja wa Stamford Bridge kuanzia dakika ya kwanza hadi tunapata ushindi, hicho ndicho nilichokuwa nataka kukifanya kwa klabu hii.

“Msimu uliopita nilikuja kwenye uwanja huo lakini matokeo hayakuwa mazuri kwangu, lakini safari hii kutokana na ubora wetu tumefanikiwa, nakumbuka nimepoteza michezo miwili yote msimu uliopita, lakini msimu huu sipo tayari kupoteza,” alisema Gaurdiola.

Hata hivyo, kocha huyo ameweka wazi kuwa alichobakisha ni kucheza na timu mbili ambazo kwake ni ngumu, Tottenham na wapinzani wake Manchester United.

“Najua nina kibarua kizito siku ambayo nitakutana na kocha Jose Mourinho na kikosi chake cha Manchester United, najua uwezo wake, najua uwezo wa wachezaji wake, wanakuwa na matokeo mazuri kila siku, wana kasi kubwa na wanaweza kupiga mipira mirefu.

“Ugumu mwingine ni kukutana na Tottenham ambayo ina mshambuliaji wake, Harry Kane, lakini nitahakikisha ninashinda michezo yote dhidi yao bila ya wasiwasi,” aliongeza.

Msimu uliopita klabu ya Chelsea ilimaliza Septemba bila ya kupoteza hata mchezo mmoja, lakini msimu huu wamejikuta wakishindwa kuipiku rekodi hiyo baada ya kichapo hicho mbele ya mashabiki wake.

Michezo mingine ya juzi ni pamoja na West Ham ikitoka na ushindi wa bao 1-0, West Brom ikitoka sare ya 2-2, Stoke City ikishinda mabao 2-1 na Leicester City ikitoka suluhu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles