25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Guardiola ahofia kufukuzwa Man City

MANCHESTER, ENGLAND 

LICHA ya Manchester City kufanya vizuri misimu miwili iliopita nchini England, kocha wa timu hiyo Pep Guardiola, ameweka wazi kuwa, anaamini muda wake wa kuishi hapo ni mfupi endapo atashindwa kufanya vizuri katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inatarajia kuendelea wiki ijayo huku Manchester City wakitarajia kushuka dimbani Februari 26 dhidi ya Real Madrid.

Manchester City msimu huu hawapo kwenye ubora wa misimu miwili iliopita ambapo waliweza kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu England mara mbili mfululizo, lakini msimu huu wanaonekana kuwa katika wakati mgumu wa kutetea ubingwa huo baada ya Liverpool kuonesha kiwango cha hali ya juu na kuongoza kwenye msimamo wa Ligi wakiwa na pointi 73 baada ya kucheza michezo 25, wakati huo Man City wakiwa na pointi 51.

Nguvu ambazo wameziweka kwa sasa Manchester City ni kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ambao hawajachukua taji hilo kwa kipindi kirefu, lakini kutokana na kiwango cha wachezaji wa Manchester City inaweza kuwa ngumu kutwaa taji hilo.

Manchester City wamekuwa na wachezaji wengi majeruhi msimu huu jambo ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa kufanya vibaya msimu huu, hivyo kocha huyo anaamini anaweza kufukuzwa kama atashindwa kufanya vizuru dhidi ya Real Madrid.

Historia ya Manchester City kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya kocha Pep Guardiola kuamzia msimu wa 2016/17 iliishia hatua ya 16 bora baada ya kuondolewa na Monaco, ikaja kuondolewa kwenye hatua ya robo fainali msimu wa 2017/18 dhidi ya Liverpool na wakatolewa tena hatua ya robo fainali msimu wa 2018/19 dhidi ya Tottenham.

“Manchester City wanataka taji la Ligi ya Mabingwa, hiyo ndio ndoto yetu, ninaamini kwenye mchezo wetu dhidi ya Real Madrid utakuwa na ushindani wa hali ya juu, lakini kama tutashindwa kufanya vizuri basi ninaamini uongozi utaniuliza maswali mengi au kufukuzwa, hivyo sijui nini kitatokea,” alisema Guardiola.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles