31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 18, 2024

Contact us: [email protected]

GPS CAR TRACKER SULUHISHO WIZI MAGARI

Vifaa vya kufatilia GPS Tracker
Vifaa vya kufatilia GPS Tracker

Na Joseph Lino,

MIAKA kadhaa iliyopita ilikuwa ni vigumu kufuatilia mali iliyoibiwa, lakini teknolojia ya ulimwengu wa sasa inazidi kurahisisha namna ya kujua eneo mali yako imefichwa au inakwenda.

Kwa Tanzania teknolojia ya kufunga mitambo ya kisasa ya GPS Car Tracking system kwenye gari imekuwepo miaka michache iliyopita. Kifaa cha GPS ambacho hufungwa kwenye gari kufuatilia mwenendo wa gari ikiwa ni njia rahisi ya kudhibiti mali kutokana na wizi au kupunguza matumizi mabaya ya gari ya kiofisi au wivu kwa wanaopendana kujua nyendo za mwenza.

Watu wengi wamekuwa bado hawana elimu ya kutosha kugundua umuhimu wa teknolojia ya Global Positioning System (GPS) kwenye magari.

Kampuni ya Mac Auto Accessories iliyoanzishwa 2013, inajishughulisha na vifaa vya magari ikiwemo kufunga kifaa cha GPS kwenye gari ambacho kinafuatilia mwenendo wa gari kwenda mahali popote nchini.

Kifaa cha GPS kinatumia mawasiliano ya satellite kufuatilia na kutoa taarifa ya mwenendo wa gari kupitia simu ya mkononi, laptop au Ipad bila kukosea.

Mkurugenzi wa Mac Auo Accessories, Edwin Temba, anaelezea Watanzania wanapaswa kufahamu usalama wa gari ili kuepuka kuingia gharama zisizo za lazima. Ukifunga GPS gari inajilinda yenyewe.

Anasema wizi wa magari umekuwa mlubwa hasa magari ya kawaida ambayo wamiliki wake ni watu wa kawaida kutokana na magari hayo vifaa vyake kuwa na soko kubwa kuliko magari yanayomilikiwa na watu wenye uwezo.

Kampuni ya Mac ikiwa na wataalamu wa vifaa vya kiusalama vya kielektroniki, inasema kifaa cha kufuatilia vyombo vya moto hasa vya usafiri vipo.

“GPS inatoa nafasi ya jinsi gani gari binafsi au kiofisi linavyoweza kulindwa bila kukupa hasara ikiwa imefungwa mitambo ya kisasa ya kiusalama,” anasema Temba.

Mbali na ufuatiliaji wa mwenendo wa magari, teknolojia hiyo pia inaweza kuzuia vitendo vya mwendo kasi kwa basi ya shule, wizi wa mafuta kwa madereva na vifaa vingine kama bajaji na pikipiki.

Temba anafafanua kuwa taasisi za kifedha hasa zinazokopesha kama Saccos zinaweza zikatumia njia ya kuwadhibiti wadaiwa sugu wa mikopo ambayo wanaweka bodi ya gari kama thamani ya mkopo.

“Taasisi za fedha kukopesha mikopo ambayo wengi huweka dhamana ya gari ikiwa atakaposhindwa kurejesha gari huchukuliwa kwa utaratibu wa kibenki kama inavyokuwa kwenye mkataba.”

Kwa maelezo ya Temba, anasema kuwa katika makubaliano na taasisi za fedha kuwa wanapata usumbufu kufualia gari ambalo limewekewa bodi.

“Huduma hii inatoa nafasi nzuri kipindi ambacho mteja ameshindwa kurejesha mkopo na wanatakiwa wachukue gari hivyo kifaa hiki kitawasaidia kutambua gari limefichwa wapi,” anaelezea.

Anasema kama mteja akifanikiwa kurejesha mkopo wote, kinatolewa kwenye gari hilo na mteja kuondoka nalo likiwa salama.

Kwa upande wa wamiliki wa shule ambazo kuna mabasi ya kubeba watoto au wanafunzi ikiwemo magari ya kiofisi ambayo yanafanya shughuli za mizunguko ya kibiashara, kifaa hiki kinasaidia.

“Kifaa hiki kinasaidia kudhibiti mwendo ambapo hutoa taarifa na basi na dereva husika mahali popote anapokwenda, hii husaidia usalama wa watoto wa shule.”

Akiongelea zaidi anasema gari likiibiwa kina uwezo wa kunasa sauti ndani ya gari ambayo inaweza kusaidia taarifa zaidi watu husika wanaofanya uhalifu.

GPS Car System kinafungwa kwa kificho ndani ya gari na kuunganishwa na mfumo wa umeme wa gari na kuwa betri ambayo hata ikizima kifaa kinaendelea kufanya kazi bila kupoteza kumbukumbu.

Unakuwa na uwezo wa kuangalia gari yako kama inaendeshwa au imezima na una uwezo wa kuizima hata kama yeye ana ufunguo wa gari.

Hili ni suluhisho kwa watoa mikopo ya magari kwani mteja mwaminifu akiweza kumaliza mkopo wake, kitasaidia kuongeza majukumu ya kulipa mkopo kwa wakati.”

Kifaa ambacho hakina gharama ya malipo ya kila mwezi kitakapofungwa na kampuni inamsaidia mteja muda wowote tatizo linapotokea.

Kwa upande wa changamoto anaelezea kuwa wamiliki wa vyombo vya moto wengi huwa na hali ya kupuuza kwamba gari haliwezi kuibiwa au watu kudhani kufunga GPS ni gharama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles