25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Gambo aonya wanaonyanyasa wanafunzi barabarani

Mwandishi Wetu, Arusha

MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, ameonya tabia ya baadhi ya madereva kuwanyanyasa wanafunzi na kuwabagua jambo ambalo ni kinyume cha sheria na taratibu za usafirishaji.

Gambo alisema hayo wakati akipokea vibao vya kuwavushia wanafunzi barabarani vilivyotolewa na Benki ya NMB na amelitaka jeshi hilo kuhakikisha kuwa wanakusanya taarifa za madereva ambao hawataki kuwapakia wanafunzi kwenye magari yao kwa kukaidi maelekezo ya bei elekezi kwa wanafunzi.

Aliwataka wanafunzi hao kutoa taarifa kwa polisi pale wanapoona kuwa wanatendewa vitendo vya unyanyasaji ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.

“Mwanafunzi ukiona wanakufanyia ndivyo sivyo andika namba ya gari fikisha kwa mzazi au peleka mwenyewe kwa polisi wa barabarani ili kukomesha vitendo hivyo, Arusha tunataka wanafunzi waheshimiwe ili waweze kusoma kwa bidii na kufaulu,” alisema Gambo.

NMB imetoa vibao 250 vya kuwasaidia kuwavusha wanafunzi ili waweze kuvuka salama na kuondokana na tatizo la ajali barabarani lililokuwa likiwakumba wanafunzi pindi wanapovuka barabara.

Gambo aliipongeza benki hiyo kwa mchango huo aliosema utapunguza ajali za barabarani na kuwahakikishia wanafunzi usalama pindi wanapovuka barabara.

Pia aliwataka madereva kuheshimu vibao hivyo na kuheshimu sheria za barabarani ili kuepuka ajali zisizokuwa za lazima.

Mkurugenzi wa Bodi ya NMB, Dk. George Mulamula, alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana vyema na polisi katika juhudi za kupunguza ajali na kuhakikisha watoto wanakuwa salama.

Alisema msaada huo unalenga kuwasaidia watoto kutimiza ndoto zao bila kukatishwa na ajali za barabarani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles