27.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Femata yaanza utekelezaji mradi wa vitambulisho kwa wachimbaji wadogo

Na Clara Matimo, Mwanza

Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania(FEMATA) limeanza utekelezaji wa mradi wa kutoa vitambulisho vya Kidigitali kwa wachimbaji wadogo kote nchini ili kutambulika rasmi, kurahisisha utekelezaji wa shughuli zao na kupata mikopo kwenye taasisi za fedha.

Makamu wa Rais wa Femata, Alfred Luvanda akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo ya mradi wa vitambulisho kwa wachimbaji wadogo Tanzania.

Utekelezaji wa mradi huo ni sehemu ya maazimio 14 yaliyofikiwa na Femata kwenye mkutano mkuu uliofanyika Mei 10,2023 jijini Mwanza.

Akizungumza kwenye uzinduzi  wa mradi huo ulioenda sambamba na utoaji mafunzo kwa Kamati Tendaji ya Femata, jijini Mwanza Juni 28, 2023  Rais wa Shirikisho hilo John Bina, alisema vitambulisho hivyo vitakuwa na faida nyingi kwa wachimbaji ikiwemo kutambulika wakati wa ajali, majanga katika migodi na sehemu yeyote hasa wakienda kufanya shugfhuli za uchimbaji nje ya nchi.

“Kupitia vitambulisho hivyo tutakuwa na database (kanzidata) ili kupata takwimu sahihi za wachimbaji wadogo na wadau wote katika mnyororo wa thamani wa madini kwa hiyo sisi wachimbaji wadogo tutatumia vitambulisho vyetu wakati wa kulipa maduhuli ya serikali au tunapokatwa tozo ama kodi mbalimbali,”alieleza Bina na kuwataka wachimbaji hao kuchangamkia fursa hiyo.

Mwenyekiti wa Miradi wa Femata, Tariq James alieleza kwamba wanatakeleza mradi huo  kwa kushirikiana na Kampuni ya MIMB/TNT Resources Ltd ya nchini Uholanzi ambapo kila mchimbaji atapata kitambulisho hicho kwa gharama ya Sh 30,000.

“Vitambulisho hivyo vitatolewa kwa wachimbaji wadogo walio kwenye mialo, maduara na wenye leseni maana tunatambua kwamba wapo wanaochimba lakini hawana leseni na mradi huu utanufaisha Shirikisho letu pamoja na vyama vya wachimbaji wadogo wa madini kwenye mikoa yote.

“Katika Sh 30,000 ambazo mchimbaji atatoa ili kupata kitambulisho, mtoa huduma atachukua Sh 18,720 zinazobaki yaani Sh 11,280 chama cha mchimbaji kitapata asilimia 60 na asilimia 40 itaenda femata ambapo kipato hicho kitaiwezesha kujiendesha na kujitegemea,”alifafanua James.

Baadhi ya washiriki wa uzinduzi wa mafunzo ya mradi wa vitambulisho vya kidijitali kwa wachimbaji wadogo wa madini Tanzania yaliyofanyika Jijini Mwanza Juni 28,2023 kwa uratibu wa Femata.

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Ndembi Tuma alisema itaendelea kutoa ushirikiano kwa Femata ili kufanikisha zoezi hilo muhimu kwa maendeleo ya sekta ya madini nchini.

“Serikali itaendelea kushirikiana na Femata kama ambavyo tumekuwa tukifanya lakini ili mradi huu ufanikiwe ni vyema mtoe elimu ya kutosha kwa wachimbaji ili wajue umuhimu wa kushiriki katika mradi huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles