27.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

EAMCEF yatoa Sh milioni 350 kuboresha uhifadhi

Na Mwandishi Wetu, Muheza

Mfuko wa Uhifadhi wa Milima ya Tao la Mashariki (Eastern Arc Mountains Conservation Endownment Fund -EAMCEF) umetoa zaidi ya Sh milioni 350 kwa ajili ya kusaidia shughuli za uhifadhi katika hifadhi ya mazingira asilia ya Amani (Amani Nature Reserve) inayopatikana katika  wilaya za  Muheza na Korogwe mkoani Tanga.

Aidha, fedha hizo zimetolewa kwa kipindi cha miaka 15 kuanzia mwaka 2006, ambazo zimetumika kwa ajili ya kusafisha mipaka, uboreshaji wa bararaba za kupita watalii,upandaji wa miche ya miti na miundombinu mingine kwa ajili ya kuvutia watalii.

Mhifadhi wa hifadhi hiyo ya mazingira ya asili ya Amani, Fikiri Maiba, amesema shughuli za uboreshaji wa mipaka ya hifadhi imesaidia kupunguza mgogoro baina yao na wananchi kwa kiasi kikubwa.

Amesema mbali na migogoro imesaidia kupunguza matukio ya uchomaji moto uliokuwa ukiingia kwa urahisi hifadhini wakati wanavijiji wanapoandaa.

“Tunapokuwa na shughuli za kusafisha mipaka na uboreshwaji wa miundombinu ndani ya hifadhi,tunawatumia wananchi wanaoishi jirani na tunawalipa hivyo inapunguza harakati za kutaka kuingia msituni kuvuna rasilimali za misitu,” amesemaMaiba.

Mbali na kutoa fedha hizo EAMCEF imeelekeza nguvu kuwawezesha wananchi wanaoishi kando ya hifadhi hiyo kupitia vikundi vyao kwa kuwapa miradi rafiki ikiwemo ya vitalu vya miti, utengenezaji wa majiko banifu na ufugaji wa nyuki.

Afisa Miradi wa mfuko huo Kanda ya Kaskazini, Magreth Victor amesema vikundi vya wananchi kupitia asasi za kiraia zinazofanya kazi kwenye maeneo husika vimekuwa vikipatiwa fedha ambazo kwa kutekeleza  miradi ya upandaji miti,utengenezaji wa majiko banifu na ufugaji wa samaki.

“Wananchi wameweza kuongeza vipato, na kupunguza kasi ya uvunaji wa rasilimali za misitu zikiwemo kuni kwa ajili ya kupikia na ukataji wa miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na kupasua mbao,” amesema.

Ametaja vijiji vya Mlesa, Kisiwani na Mashewa kuwa ni miongoni mwa vijiji vinavyotekeleza baadhi ya miradi ya upandaji wa miche ya miti ya viungo na utengenezaji wa majiko banifu ambavyo washirika wake wengi ni wanawake ambao wameweza kuondokana na utegemezi.

 Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake cha Kazamwendo, Nietiwe Robert, amesema wanajishughulisha na uandaaji wa miche ya miti ya viungo ikiwemo karafuu na mdalasini.

“Tumeanza shughuli ya bustani kuanzia mwaka 2007,tunashukuru mradi kwa kweli kwani umetusaidia kujiinua kiuchumi kuna wengine wameweza kununua mashamba,kupeleka watoto shule na kuanzisha miradi mingine ya kiuchumi,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles