27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Mwele Malecela afariki dunia, Rais Samia amlilia

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkurugenzi, Mpango wa Magonjwa ya Kitropiki Yasiyopewa Kipaumbele wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk.Mwele Malecella amefariki dunia akiwa kwenye matibabu nchini Geneva
Mei 18, 2019 saa 6:45 Dk. Mwele kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter aliandika “Ni mwaka mmoja sasa tangu nigundulike nina saratani, nimepata mafunzo na baraka. Namshukuru Mungu.

Kufuatia kifo hicho Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ambapo amesema kuwa:
“Nimesikitishwa sana na kifo cha Dkt Mwele Malecela, mwana wa Afrika ambaye ameitumikia vyema Tanzania ndani na nje ya mipaka. Pole zangu zimfikie Mzee John Malecela na familia yake yote wakati huu wa majonzi mazito.
“Mungu ailaze roho yake mahali pemapeponi
,” ameandika Rais Samia ambaye yuko ziarani nchini Ufaransa na baadae Ubelgiji.

Dk. Mwele alizaliwa Machi 26, 1963, alilwahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimri) pia aliwania nafasi ya mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Desemba 16, 2016 Hayati Rais John Magufuli alitengua uteuzi wake wa Ukurugenzi wa NIMRI ikiwa ni siku moja tangu Dk. Mwele aeleze kuwa ugonjwa wa Zika upo nchini.

Hata hviyo, Aprili 2017 Dk. Mwele aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Espen), wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Dk. Mwele Malecela anayeshughulikia magonjwa yasiyopewa kipaumbele (NTD) akisimamia miradi ya kupunguza magonjwa ya Kitropiki yasiyopewa kipaumbele katika nchi 149 duniani, nafasi ambayo ameitumika hadi mauti yalipomkuta leo hii Februari 10, 2022.

Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni pamoja na matende, mabusha, kichocho, minyoo ya tumbo na usubi.

a Binadamu (Nimri)

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles