24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kijaji ataja vipaumbele 10 mwaka wa fedha 2023/24

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

WIZARA ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imetaja vipaumbele vyake 10 katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikiwemo kuboresha mazingira ya biashara nchini.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Mei 4,2023 Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Ashatu Kijaji wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo bungeni kwa mwaka wa fedha 2023-2024.

Wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa zaidi ya Sh bilioni 119 ambapo zaidi ya Sh bilioni 75 ni kwa matumizi ya kawaida na zaidi ya Sh bilioni 63 ni mishahara na zaidi ya Sh bilioni 43 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Dk. Kijaji amevitaja vipaumbele vya wizara hiyo kuwa ni kutekeleza miradi ya kielelezo ya Magadi Soda Engaruka, Makaa ya Mawe – Mchuchuma na Chuma-Liganga.

Pia, uwekezaji katika maeneo maalum ya kiuchumi (SEZ) na kongani za viwanda ikiwa ni pamoja na Nala SEZ, Kwala SEZ, Mkulazi SEZ, eneo maalumu la uwekezaji Bagamoyo;

“Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma.Kuboresha Mazingira ya Biashara.Kukuza Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi. Kukuza Sekta Binafsi.Kuratibu majadiliano ya biashara baina ya nchi na nchi, Kikanda na Kimataifa na Kuimarisha Huduma za Biashara na Masoko,” amesema Dk. Kijaji.

MALENGO

Dk. Kijaji amesema katika mwaka wa 2023/2024 Wizara imepanga kukamilisha Sera, Mikakati na Miongozo ya kuendeleza sekta ya Viwanda, kuboresha na kuongeza ustawi na tija ya viwanda nchini.

Pia, kuwa na takwimu, tathmini na taarifa zitakazowezesha kuendeleza sekta ya Viwanda,kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vipya na kongani za viwanda,kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kimkakati na kielelezo.

Vilevile,kufanya majadiliano na mwekezaji ili kusaini Mkataba wa ubia pamoja na kulipa leseni za uchimbaji wa Makaa ya Mawe Katewaka,kufanya utafiti wa kina wa kijiolojia (Geological study) na kulipia leseni za uchimbaji katika Mradi wa Makaa ya Mawe Muhukuru.

“Kuendeleza kiwanda cha KMTC katika Mkoa wa Kilimanjaro,kuendelea na ujenzi wa miundombinu ya msingi katika Kongani ya Viwanda – TAMCO,Kuendeleza Kiwanda cha TBPL na kuendelea kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa,”amesema Waziri huyo.

Ameyataja malengo mengine ni kukamilisha majadiliano na mwekezaji na kusaini mkataba wa ubia (JVA Agreement) na kulipia leseni za uchimbaji – Maganga Matitu.

“Kutafuta mwekezaji na Kufanya ukarabati wa majengo katika kiwanda cha Mang’ula,Kufanya maandalizi ya awali kwa mradi wa mafuta ya kula (preliminary preparation for establishment of edible oil) na kuendelea kufanya ukarabati wa majengo ya Nyanza Glass ili kuvutia wawekezaji wa viwanda,”amesema Dk. Kijaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles