Mohamed Hamad, Manyara
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Tumaini Magesa amewataka wananchi wa Kijiji cha Ilkiushbor kuuza mifugo yao na kujenga mabweni ili watoto wao waondokane na adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.
Akizungumza na wananchi wa Kijiji hicho Magesa amesema watoto wengi wilayani humo hawaendi shule kutokana na umbali ambapo hutumia muda mwingi njiani wakielekea shuleni.
“Hali hiyo imesababisha utoro ambapo wengi wao huacha shule pamoja na wengine hupata mimba za utotoni,” amesema.
Kutokana na hali hiyo, Magesa amesema jitihada za Serikali ni kuhamasisha wananchi kujenga mabweni hadi kufikia hatua ya kuezeka kisha wao watamalizia.