Na Denis Sikonde, Songwe
Mkuu wa Wilaya ya Ileje mkoani Songwe, Anna Gidarya amewataka vijana wanaohitimu mafunzo ya jeshi la akiba wilayani humo kutumia mafunzo hayo kulinda usalama wa raia na Mali zao na si kuyatumia kunyanyasa wananchi.
Gidarya amesema hayo Novemba 10, 2022 wakati akifunga mafunzo ya jeshi la akiba Kwa vijana 104 yaliyokuwa yakiganyika katika Kijiji cha Sange kata ya Sange Tarafa ya Bundali wilayani humo.
Gidarya amewataka wahitimu hao kutumia mafunzo hayo kulinda mipaka ya nchi, usalama wa Mali za wananchi na kutambua suala la ulinzi ni jukumu la raia wote.
Gidarya amesema kuwa ana imani kuwa mafunzo hayo yamewajenga vijana ukakamavu ujasiri na kujiamini kwani kwa sasa wahitimu watakuwa tofauti na waliokimbia mafunzo haya.
“Nina imani ndugu zangu mafunzo haya yatawasaidia sana kwenye ukakamvu kwani mtakuwa ni tofauti kabisa na wasio fanya mafunzo ya mgambo kwani kwa sasa mtakuwa na hali ya kujiaminina kuwa wajasiri kutokana na mafunzo mliyopata,” amesema Gidarya.
Kwa upande wake Mshauri wa Jeshi la Akiba wilayani humo, Winfred Msheri amesema kuwa mafunzo hayo yalianza yakiwa na jumla ya wanafunzi 135 na ilipungua hadi kufikia 104 wakiwepo wanawake 8 wamehitimu kwani wengine walishindwa kumaliza mafunzo hayo kutokana na sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na utovu wa nidhamu.
“Mheshiwa mgeni rasmi kuwepo kwa idadi ndogo ya wahitimu wa mafunzo hayo yametokana na jamii kuwa kuwa na Imani potofu kwamba mafunzo hayo ni mateso Hali iliyopelekea baadhi ya vijana kukimbilia wilaya jirani na mikoa jirani kukimbia mafunzo hayo,” amesema Msheri.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya jeshi la akiba, Shangwe Msokwa mafunzo yamewajengea ukakamavu, uzalendo kwa ujumla hivyo ameahidi kuwa watayatumia mafunzo hayo kwa masilahi mapana ya Taifa