Na AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM
DAKTARI Bingwa wa Macho katika Hospitali ya Macho (CCBRT) Dk Cyprian Ntomoka amesema kuwa utafiti uliofanywa unaonesha kuwa Bilinganya inauweza kuongeza kiwango cha uoni endapo itatumiwa katika milo.
Dk Ntomoka aliyasema haya jana jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano maalum na Gazeti la MTANZANIA ambapo alisema ni muhimu watu kutumia katika kuongeza kiwango cha uoni na kuepuka ugonjwa wa presha ya macho.
“Kunatafiti ambazo zimeonesha kuwa bilinganya inachemikali ambayo inasaidia kupunguza presha ya jicho.
“Jicho lina presha na presha ya jicho inasababishwa na maji kuwa mengi kwenye jicho ambayo huweza kuwa sababu tatizo katika jicho, huwa maji yanatoka na kuingia sasa yakiingia mengi yakatoka kidogo tatizo huanzia hapo tunasema mtu anashinizo la jicho.
“Maji yakijaa ndani yanaumiza jicho na ugonjwa hauwezi kuonesha kwani dalili ya kwanza na ya mwisho ni kupoteza uwezo wa kuona kabisa,” alibainisha.
Alisema aina ya kemikali inayopatikana kwenye bilinganya inasaidia kupunguza kiwango cha maji maji yanayoingia kwenye jicho na kutengeneza uwiano ulio sawa.
“Maji yanayotoka kwenye jicho yanapimwa na uwezo wa kutolea maji wengi tunaowatibu tunawapa dawa za kupunguza maji ili iwepo balance cha kiwango cha maji
“Wagonjwa wengi ni kwasababu ya uzee kuanzia miaka arobaini chekecheo cha maji kinapungua pia huu ugonjwa unarithiwa kutoka kwa ndugu Kwahiyo biringanya inapunguza kiwango cha maji,” alisema .
Alitoa ushauri kwa watu kutumia bilinganya ili kuweza kupunguza kiwango cha majimaji katika jicho na kusaidia katika kuongeza kiwango cha uoni hivyo kufanya jicho kuwa salama.
“Hapa CCBRT kwa idadi ya wagonjwa wanaokuja tuna kliniki tatu za kuona ugonjwa wa presha ya macho kwa siku kati ya wagonjwa 30 hadi 40 wanakuja kufatilia matibabu ya presha ya macho kwahiyo kwa wiki wagonjwa tunawaona 120 kati ya asilimia 5 na 10 hili ni tatizo kubwa.
Alishauri watu kupunguza kula vyakula vya wanga badala yake wale vyakula vyenye virutubisho .
“Kuna watu wanaona kuwa mboga za majani ni umasikini lakini ndio zenye vitamin lakini pia na matunda hasa yenye vitamin C vinasaidia, watu wasipende kula nafaka ambayo imekobolewa kwani vimetolewa kiini na ganda ambavyo vinavirutubisho kwaajili ya macho,” alishauri.