Havana, Cuba
Rais wa Cuba, Miguel Diaz-Canel ametangaza dozi ya tatu inayoitwa Abdala ya chanjo dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona imethibitishwa kuwa na ufanisi wa 92.28% katika awamu ya tatu ya majaribio yake.
Tangazo hilo limekuja baada siku kadhaa baada ya serikali ya Cuba kusema kuwa chanjo nyingine iliyotengenezwa nchini humo inayoitwa , Soberana 2, ilikuwa na ufanisi wa 62% kwa dozi mbili tu kati ya tatu.
“Kwa kuathiriwa vibaya na janga la corona, wanasayansi wetu, katika Taasisi ya Finlay na kituo cha uhandisi wa Jeni na teknolojia ya kibaiolojia wameweza kupita vikwazo vyote na kutupatia chanjo zenye ufanisi mkubwa ,” aliandika Rais Miguel Diaz-Canel kupitia Ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii Twitter.
Pia tangazo hilo limetolewa baada ya lile la Shirika la madawa la taifa Bio Cuba Farma, linalosimamia Finlay, ambao ni watengenezaji wa Soberana 2, na Kituo cha uhandisi wa Jeni na teknolojia ya kibaiolojia (Center for Genetic Engineering and Biotechnology, ambao ni wazalishaji wa chanjo ya Abdala.
Chanjo zote zinatarajiwa kupewa mamalaka za dharura na taasisi ya usimamizi wa viwango muda mfupi.
Nchi ya Cuba, ambayo sekta yake ya teknolojia ya baiolojia imekuwa ikituma nje ya nchi chanjo kwa miongo kadhaa, ina chanjo tano za corona zinazofanyiwa majaribio.