Nairobi, Kenya
Maafisa wa Afya nchi Kenya wametoa ripoti ya kuathiriwa kwa mfumo wa uchangiaji damu ulisababishwa na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19.
Ripoti hiyo imekuja baada ya wachangiaji damu waliopata sehemu ya Kwanza ya chanjo ya Covid 19 ya Astra Zeneca wanapaswa kusubiri siku saba kabla ya kuchangia damu.
Huduma ya Kitaifa ya Uchangiaji Damu nchini humo hukabiliwa na changamoto ya kufikia lengo la kukusanya damu pointi milioni moja kila mwaka.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kipindi cha kuahirisha utoaji damu kinawapatia furasa wachangiaji kutathmini ikiwa wana athari yoyote baada ya chanjo.