24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Compassion International Tanzania lapongezwa Iramba

Na Seif Takaza, Iramba

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Kikiristo la Compassion International Tanzania na Ushirika wenza wa Makanisa sita Klasta ya Iramba mkoani Singida limepongezwa kwa kuwahudumia Watoto na vijana wanaoishi katika mazingira magumu.

Pongezi hizo zimetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleimani Mwenda katika kikao cha wadau cha Utambulisho wa huduma ya Maendeleo ya Mtoto na Kijana  kilichofanyika mjni Kiomboi ambapo wadau mbalimbali walihudhuria wakiwemo baadhi ya madiwani wa Halmashauri, baadhi ya wakuu wa idara na Wachungaji wa makanisa sita waliopo kwenye Mpango.

Mwenda amesema Shirika hilo limekuwa na ufariji mkubwa kusaidia  Watoto na vijana ambao wazazi na walezi wao wana hali mbaya kiuchumi.

“Mimi shuhuda kuhusu Shirika hili la Compassion ambalo linasaidia sana Watoto na vijana wanaoishi katika mazingira magumu kwa kweli linanipa Faraja kubwa katika Wilaya yangu, hivyo sisi ni wajibu wetu kiwaunga mkono kwa hali na mali.

“Changamoto ya kukosa ushirikiano siku ya Jumamosi kwa ajili ya kutoa mafunzo ya malezi, elimu ya mazingira na kumtambua Mungu wao kwa ajili ya kuandaa kizazi kilicho bora ataifanyia kazi ili lengo la Shirika hilo na washirika wenza katika Makanisa sita yaliopo katika Program hiyo itimie,” alisema Mwenda.

Kwa Upande wake Mwezeshaji wa Shirika hilo wa Klasta za Iramba na Mkalama, Raphael Lyela amesema Shirika La Compassion limeanza Novemba 2014 ambapo lengo lake ni kuwahudumia Watoto na vijana waishio katika mazingira magumu.

Lyela alitaja vituo vilivyopo katika Klasta ya Iramba ni TAG Kiomboi, EATG Kiomboi, FPCT Shelui, KKKT Shelui, TAG Kinampanda na TAG Ulemo ambapo kila Kanisa lilipatiwa Watoto 200.

“Tumekuwa tukiwafundisha Watoto na vijana masomo mbalimbali kama vile masomo ya Kiuchumi ili kuhakikisha Watoto wanakuwa na stadi za maisha waweze kumudu mazingira yao na kujitegeme , Kijamii kuhakikisha vijana wanakuwa na tabia njema katika jamii na kimwili vijana wanakuwa na afya njema pamoja na kiroho ambapo vijana wanakua na hofu ya Mungu na maadili mema katika jamii,” alisema Lyela.

Lyela amesema huduma hizo zimegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni huduma ya kunusuru maisha ya mama na mtoto na huduma ya ufadhili kwa watoto kuanzia miaka mitatu na kuendelea.

Naye Yohana Kamwela ambaye ni Mwenyekiti wa Klasta ya Iramba akitoa taarifa yake ambapo alisema kuwa katika Progamu zote mbili ina jumla ya washiriki 1569 katika vituo kama ifuatavyo TAG Kinampanda 258, TAG Ulemo 261, TAG Kiomboi 243, EATGKiomboi 231, FPCT Shelui 241 na KKKT Shelui 245.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles