29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Chama cha Wanasheria Wanawake watoa Mafunzo

Janeth Mushi, Arusha

CHAMA Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (Tawla), tawi la Arusha, kimetoa mafunzo kwa bodi, menejimenti kutoka taasasi za kiraia sita,b majukwaa ya uwezeshaji ya wanawake na vijana juu ya uongozi na usimamizi.

Akizungumza jana katika mafunzo hayo,Msimamizi wa Programu kutoka makao makuu ya chama hicho,Wakili Mary Richard,alisema mafunzo hayo yamelenga kuhakikisha taasisi hizo zinakidhi mahitaji ya kisheria,kanuni na taratibu ambazo zimewekwa na serikali.

Amesema mafunzo hayo kwa mashirika hayo yasiyo ya kiserikali,yametolewa kupitia mradi wake wa IDIET,ambao wanautekeleza katika mikoa mbalimbali chini ya ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).

“Tumekutana kukumbushana na kuangalia masuala ya uongozi na usimamizi na masuala ya kuhakikisha taasisi zinakidhi mahitaji ya kisheria  na kanuni ambazo serikali zimeweka kwenye usimamizi wa fedha na utawala kwa ujumla,”alisema

“Ili muweze  kufanya kazi kikamilifu ni lazima mfahamu majukumu yenu,kwani ukishafahamu jukumu  lako litakupeleka kujua nyenzo za kufanyia majukumu yako ni zipi,nyenzo ambazo ni sheria,kanuni na taratibu za serikali na sheria na kanuni za taasisi,”

“Kimsingi hapa tulikuwa tunakumbushana wajibu wa wajumbe wa bodi na mashirika na menejimenti na namna ya kuangalia mipaka yao,sheria,kanuni na taratibu ni zipi za serikali na zilizopo kwenye taasisi zetu wenyewe,”aliongeza

Kwa upande wake Katibu Mkuu kutoka Shirika la Emayani Foundation,Wakili Sylvia Mwanga,ameomba asasi,taasisi na mashirika madogo kujengewa uwezo wa kutengeneza sera ili ziwasaidie katika shughuli zao.

Amesema kupitia mafunzo hayo wamefahamu umuhimu wa kuwa na sera ambazo zinaendesha majukumu ya shirika kwani mashirika mengi hasa madogo yanajiendesha bila sera.

“Kupitia mafunzo haya tumejengewa uwezo kwenye masuala ya uongozi,kazi bodi za mashirika mbalimbali,tumejifunza umuhimu wa kuwa na sera ambazo zinaendesha majukumu ya shirika,”

“Sera hizi zimeonekana mashirika mengi hayana kutokana na kutokutambua umuhimu wake na kazi zake katika uendeshaji wa mashirika,tunaomba tujengewe uwezo wa kutengeneza sera ikiwemo ambazo zinasaidia kuweka  utaratibu mzuri wa kujiendesha,”ameongeza

Wakili huyo alisema kukosekana kwa sera hizo kunasababisha mambo mengi ikiwemo baadhi ya mashirika kukosa wafadhili ambao wangeweza kuwasaidia endapo wangekuwa na sera mbalimbali za kujiendesha.

“Kutokana na hilo tumeona ni muhimu zaidi kuhakikisha mashirika yanajengewe uwezo kipengele cha kutengeneza sera ili kuhakikisha zinawapeleka katika njia ambazo hazitakinzana na sheria za nchi  lakini pia zitarahisisha uendeshaji kazi wao,”

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Youth and Child Center iliyopo wilayani Karatu,Kiliani Melkiori,amesema mafunzo hayo yametolewa kwa wakati muhimu na kuwa yatawasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi bila kukiuka kanuni,taratibu na sheria za nchi.

 “Tumejifunza na kukumbushana juu ya masuala mbalimbali ikiwemo  namna ya kusimamia shughuli kwa mgawanyo,umuhimu wa sera na masuala mengine ambayo hatukuwa nayo kwenye taasisi zetu,”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles