29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

CERF yatenga dola milioni 26.5 kwa ajili ya Sudan

Wakimbizi wa ndani jimbo la Darfur Sudan wanakabiliwa na changamoto nyingi na ugumu wa kupata maji safi. Pichani ni msichana na kaka yake wakiwa katika kituo cha maji safi cha Abu-Shok kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani illi kuteka maji

Wakati huo huo Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA, Mark Lowcock ametangaza kutengwa kwa dola milioni 26.5 kwa ajili ya msaada wa dharura, CERF kwa ajili ya kuwasilisha chakula, lishe, huduma ya afya, maji na huduma ya kujisafi kwa takriban watu 800,000 walioathirika na janga la kiuchumi na chakula linaloshuhudiwa katika majimbo saba Sudan kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita.

Bwan Lowcock kupitia taarifa ya OCHA amesema, “janga la kiuchumi linaloshuhudiwa limekuwa na athari zinazokwenda mbali ya uhakika wa chakula.

Ongezeko la bei ya chakula inamaanisha kwamba familia zinakulwa chenye upunugfu wa ubora na watoto wengi wachanga na wanawake wajawazito wanaugua. Familia zinakabiliwa na wakati mgumu na wanashindwa kupata tiba, isitoshe kupoteza ajira kunawalazimu kuondoa watoto wao kutoka shule.

Mgao huo wa CERF unalenga wakimbizi wa ndani, wakimbizi na jamii zinazowahifadhi pamoja na wakazi walio hatarini katika maeneo kunakoshuhudiwa ukosefu wa chakula toshelezi ikiwemo, mashariki, kaskazini, kusini na Darfur magharibi, Red Sea, Kordofan magharibi na majimbo ya White Nile.

Ukosefu wa chakula umeongezeka huku ikikadiriwa kwamba watu milioni 5.8 hawana chakula toshelezi tangu Jamuari hadi Machi hii ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishw ana mwaka 2018.

Huduma za ulinzi zitapewa kipaumbele kwa ajili ya mahitaji ya watoto, wanawake na waliohatarini ikiwmo watu wanoishi na ulemavu na walio na magonjwa ya muda mrefu.

Licha ya fedha hizo na zingine kutoka mfuko wa misaada ya kibinadamu ya Sudan dola milioni 21 bado mahitaji ya kifedha hayatoshelezi kufuatia ongezeko la mahitaji. Mwaka huu wa 2019, Umoja wa Mataifa unatarajia kutoa ombi la dola bilioni 1 kwa ajili ya kusaidi watu milioni 4.4 walio hatarini nchini Sudan.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles