28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Bunge kupokea Muswada wa Sheria ya Habari

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limeeleza kuwa macho na masikio ya wadau wa habari nchini, yanaelekezwa jijini Dodoma kusubiri muswada wa Sheri ya Habari ukisomwa kwa mara ya kwanza Januari hii.

Mwenyekiti wa Jukuwaa la Wahariri Tanzania(TEF), Deodatus Balile.

Hayo yamebainishwa mapema leo Alhamisi Januari 19, 2023 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile ambapo amesema kuwa hatua iliyofikiwa ni nzuri na maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan yanatekelezwa na shauku kubwa ya wadau wa habari nikuona muswada huo ukiwasilishwa bungeni Januari hii.

“Wiki hii tunarajia kwamba Wizara ya habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari itawasilisha muswada wa huduma za habari bungeni na utajadiliwa na Mungu akipenda mwezi Febuari utakua umepitishwa kuwa sheria na tumeona kwamba mwelekeo ni mzuri.

“Hivyo, TEF pamoja na wadau wote wa habari tunatarajia kwamba mambo yatakwenda vizuri endapo muswada huo utaingia bungeni na kusomwa kwa mara ya kwanza,” amesema Balile.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles