Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
BENKI Letshego na TCB Bank zimeingia mkataba maalum kuhakikisha wateja wao wanapata huduma bora na za uhakika za kifedha.
Akizungumza leo Dar es Salaam Mei 10, katika mkutano na waandishi wa habari Mkurungenzi Mtendaji wa TCB, Jeremian Msuya amesema mkataba huo wa kibiashara umetokana na maombi ya wateja wao ili kuweza kupata huduma za kifedha nchini.
“Kwa Sasa mteja wa benki ya letshengo na TCB benki ataweza kuweka pesa na kutoa pesa katika matawi 82 nchini,” amesema Msuya.
AmesemamMuungano huu upo katika mfumo wa tehama na unamuwezesha mteja wa benki zote mbili kupata huduma anayostahili.
Naye Mkurugenzi wa Bodi ya Benki Letshego, Saimon Jengo amesema huduma inayozinduliwa leo itamuwezesha Mteja kupata huduma za kibenki kupitia taasisi hizo mbili.
Amesema benki hiyo ambayo inamuwezesha mfanyabiashara kuweza kutoa mkopo wa kibiashara na kuweza kukuza uchumi wa biashara yake.
Amesema kwa sasa mteja ataweza kuhudumiwa na mawakala zaidi ya 5,000 kwa ushirikiano wa TCB na Let Shengo banki kwa kufanya muamala ya kuweka na kutoa pesa.