Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Benki ya Akiba Commercial (ACB) imesema itaendelea kutunza na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya urithi bora wa vizazi vijavyo.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, Meneja wa Benki ya Akiba Tawi la Dodoma, Upendo Makula, amesema amesema jitihada hizo zinakwenda sambasamba na kaulimbiu ya mwaka huu, isemayo ‘Ardhi Yetu, Mustakabali Wetu’ ambayo inalenga urejeshaji wa ardhi na kupambana na majanga.
Katika kusherehekea siku hiyo benki hiyo pia imekabidhi awamu ya pili ya uboreshaji wa viwanja vya Independence Square vilivyopo jijini Dodoma jukumu ambalo limekuwa likitekelezwa na Akiba kwa zaidi ya miaka 10.
“Ni wajibu wa kila mmoja kulinda na kuhifadhi mazingira ili kuhakikisha dunia inabaki kuwa mahali salama pa kuishi kwa sasa na vizazi vijavyo. Benki ya Akiba inashiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira kwa namna mbalimbali kuanzia kupitia huduma zake na ushiriki wake katika shughuli za kijamii,” amesema Makula.
Meneja huyo amesema benki hiyo imepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya karatasi kwa kuboresha huduma zake za kidijitali zikiwemo Akiba Mobile, Akiba Wakala, kadi za VISA, taarifa za kielektroniki (E-statement) na huduma za benki Mtandao (Internet Banking).
“Huduma hizi si tu kwamba zinapunguza matumizi ya karatasi, bali pia huleta urahisi na uhakika, hivyo kukidhi mahitaji ya soko kwa ufanisi,” amesema.
Benki hiyo pia inatoa huduma mbalimbali kama mikopo, akaunti na bima zinazowafikia wateja tofauti kuanzia mtu binafsi hadi makampuni makubwa na taasisi za serikali.
Vilevile inashiriki kikamilifu katika shughuli za jamii za kuhifadhi mazingira kama sehemu ya Sera yake ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).
Hafla hiyo pia imehusisha kupanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vilivyoboreshwa vya Independence Square.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma ambaye alikuwa mgeni rasmi, Jabir Shakimweri, ameipongeza Benki ya Akiba kwa juhudi zake za kuboresha na kuhifadhi mazingira na kutoa rai kwa taasisi zingine kuiga mfano h