27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Baraza la kijeshi lawakamata maafisa wa zamani

KHARTOUM, SUDAN

BARAZA la mpito la kijeshi nchini Sudan limewakamata waliokuwa maafisa wa serikali na kuahidi kutowatawanya waandamanaji.

Msemaji mmoja pia ameuomba upinzani kumchagua waziri mkuu mpya na kuahidi kumwidhinisha watakayemchagua.

Maandamano ya miezi kadhaa nchini hapa yamechangia kutimuliwa kwa kiongozi aliyekaa muda mrefu madarakani, Omar al-Bashir Alhamisi wiki iliyopita

Lakini waandamanaji wameapa kusalia mitaani mpaka itakapoundwa serikali ya kiraia

Raia wanaendelea kuandamana na wamepiga kambi nje ya makao makuu ya wizara ya ulinzi katika mji mkuu Khartoum.

Katika mkutano na wanahabari juzi, Msemaji wa Jeshi, Meja Jenerali Shams Ad-din Shanto alieleza kuwa baraza la kijeshi lipo ‘tayari kuidhinisha’ serikali yoyote ya kiraia itakayoidhinishwa na vyama vya upinzani.

“Hatutomteua waziri mkuu. Watamchagua wenyewe,” alisema akimaanisha upinzani na makundi yanayoandamana.

Ameeleza pia kwamba jeshi halitawaondoa waaandamanaji kwa lazima lakini ametoa wito waruhusu maisha kuendelea kama kawaida na waache kuweka vizuzi kinyume cha sheria.

“Kushika silaha hakutoruhusiwa,” aliongeza

Baraza la kijeshi pia limetangaza baadhi ya maamuzi yakiwemo: Viongozi wapya wa jeshi na polisi, mkuu mpya wa kitengo cha ujasusi (NISS), Kamati za kupambana na rushwa na kuchunguza chama tawala kilichoondoka

Mengine ni kuondolewa kwa marufuku zote na kubanwa kwa vyombo vya habari, kuachiwa kwa maafisa wa polisi na jeshi waliozuiwa kwa kuunga mkono waandamanaji; ukaguzi wa wawakilishi wa kidiplomasia, na hatua ya kutimuliwa kwa balozi wa Sudan nchini marekani na Uswisi.

Maandamano ya kupinga kupanda gharama ya maisha yalianza Desemba mwaka jana lakini punde tu yakageuka kuwa wito wa kumpinga Rais Bashir na utawala wake wa miaka 30.

Aliyeongoza mapinduzi hayo, Waziri wa Ulinzi, Awad Ibn Auf, alitangaza jeshi litasimamia serikali ya mpito kwa kipindi cha miaka miwili kitakachofuatiwa na uchaguzi na akaidhinisha miezi mitatu ya hali ya dharura.

Lakini wandamanji waliapa kubakia mitaani hata baada ya hatua hiyo, wakitaka mageuzi na kuidhinishwa kwa serikali ya kiraia mara moja.

Ibn Auf himself alijiuzuliu siku ya pili, kama alivyojiuzulu mkuu wa usalama anayeogopwa na wengi Jenerali Salah Gosh.

Luteni Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan baada ya hapo alitajwa kuwa kiongozi wa baraza la mpito la kijeshi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles