32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Balozi Dk. Kusiluka aipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu

*Ni kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa mji wa Serikali

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dk. Moses Kusiluka ameipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Uratibu na Usimamizi mzuri wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dk. Moses Kusiluka akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wakati wa ziara ya mji wa Serikali mtumba jijini Dodoma.

Ametoa pongezi hizo mapema leo, Oktoba 5, 2023 alipokuwa katika ziara maalum ya Makatibu Wakuu ya kutembelea mji wa Serikali Mtumba Dodoma ambapo alisema mafanikio ya mradi huo wa ujenzi wa Mji wa Serikali ni kukamilika kwa ukamilifu wake akitolea mfano ujenzi wa Uwanja wa Mashujaa kuwa ni alama kubwa ambao utatumika kwa mambo mengi ikiwa ni pamoja na wageni kujifunza nini ambacho Tanzania imefanya.

“Tunathamini kazi yenu kubwa sana mnayofanya, kama tulivyosema awali kwenye Wasilisho, hii kazi inahitaji Uratibu kwa sababu ni kazi ya Serikali, siyo kazi ya mmoja kuwa amemaliza na wengine kujisikia vibaya, tunashukuru kwa kutupitisha kwenye kazi kuanzia mwanzo, tumeona juhudi kubwa za wataalamu wetu na wasimamizi lakini pia tumeona kazi kubwa iliyopo mbele na tunatambua kwamba baadhi ya wadau wanakaribia kumaliza kazi zao,” alisema Balozi Dk. Kusiluka.

 Aliendelea kusema kuwa bado kuna muda wa kutosha wa kutatua changamoto ndogo zilizobainika katika ziara hiyo; na kusisitiza kuutazama mradi huo kwa ujumla wake kama Serikali moja, na kazi ya uratibu ikiendelea lakini pamoja na kuimarisha timu ya wataalamu wa ngazi zote katika ujenzi na kuwasikiliza:

“Ni fursa pekee ambayo tumepewa ya kujenga Makao Makuu ya Serikali mapya na serikali imetoa fedha nyingi kwa hivyo ni lazima sisi wataalam tufanye kazi inavyopaswa,” alisisitiza.

Alimshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huo, na kuwapa uhuru wataalam kufanya kazi ya kitaalam inavyopaswa, na kushauri wadau wengi kushiriki katika kazi hiyo pamoja na kujadili mambo ya kitaalam ili watu wengi waweze kujifunza

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Dk. Jim Yonaz alisema swala la ushirikishwaji wa wataalam katika ujenzi wa mji wa Serikali ni swala la muhimu sana, na wadau mbalimbali wanashirikishwa kwa ajili ya kuja kuwekeza katika maeneo mbali mbali ambayo yametengwa katika mji huo wa Serikali na majengo hayo ya yapo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles