24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

AUSTRALIA YAPATA WAZIRI MKUU MPYA

CANBERRA, AUSTRALIA              |                     


CHAMA cha Liberal nchini Australia kimetangaza kumteua Scott Morrison kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, kuchukua nafasi ya Malcolm Turnbull, ambaye hadi ameondoka alikuwa kwenye shinikizo kubwa la kupigiwa kura za kutokuwa na imani naye.

Mzozo wa uongozi uliokikumba chama hicho ulisababisha kufikia hitimisho la kuamua kuitisha uchaguzi. Walimchagua Scott Morrison, ambaye ni Mwekahazina kwa kura 45, huku mpinzani wake, Peter Dutton akipata kura 40.

Morrison anakuwa Waziri Mkuu wa 30 katika taifa hilo ambalo limeendelea kushuhudia mzozo wa uongozi ndani ya miaka 10 hadi sasa.

Mwanasiasa kinara wa chama hicho, Nola Maroni,  amesema kuchaguliwa kwa Morrison, ambaye alipata kura 45 kati ya 50 dhidi ya waziri wa mambo ya ndani Peter Dutton ni mwelekeo mpya baada ya Turnbull kutowania tena kwenye uchaguzi huo.

Turnbull alikuwa akipuuzia wito wa kumtaka ajiuzulu wakati tuhuma za uongozi zikiididimiza serikali yake.

Morrison aliwahi kuwa mkurugenzi wa mamlaka ya utalii nchini humo, ambaye ameshikilia wizara kadhaa, zikiwamo za uhamiaji na huduma kwa jamii.

Alipata umaarufu alipokuwa waziri wa uhamiaji katika serikali ya waziri mkuu wa zamani, Tony Abbott. Anasifika kuwa kiongozi asiyetaka upuuzi katika kuidhinisha sera kali ya Australia ya kusitisha uhamiaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles