24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Auawa kwa tabia za ubakaji, wizi

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei.

Na Ramadhan Libenanga, Morogoro

MKAZI wa Kijiji cha Ulaya, wilayani Kilosa mkoani hapa, Siawana Rashid ameuwawa na wananchi kwa madai ya tabia za ubakaji, wizi na kupiga watu.

Tukio hilo limetokea Septemba 9, mwaka huu katika  Kijiji cha Nyali Kanisani, ambako marehemu alifanya tukio la wizi alikamatwa na kupigwa hadi kupoteza maisha na wakazi wa maeneo hayo.

Diwani wa Kata ya Ulaya, Matokeo Erasto, alisema kwa miaka mingi marehemu amekuwa akisumbua wananchi kwa kushiriki matukio ya ubakaji na ujambazi kwa nyakati tofauti.

“Pamoja na kufanya matukio yote hayo na kuripotiwa kwenye vyombo vya usalama alikuwa anakamatwa na muda mchache anaachiwa hali ambayo iliwakatisha tamaa wananchi wa kata hii hadi kufikia hatua ya kumuua,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mkanda B, Nashon Masasi alisema  siku ya tukio marehemu alifanya matukio matatu ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kupiga na kujeruhi na kuchoma moto milango ya nyumba ndipo alipokamatwa na kuvamiwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio na ambapo alitoa onyo kwa watu wenye tabia za wizi na kuisumbua jamii kuacha tabia hizo kwani ni kinyume na sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles