25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Askofu wa Wasabato aelezea maombi ya JPM

Na AVELINE KITOMARY, DAR ES SALAAM

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Waadventist Wasabato Jimbo  Kuu la Kusini, Mark Marekana, amewataka Watanzania kuwa na mtazamo chanya katika maombi ya shukrani ya siku tatu yaliyotangazwa na Rais John Magufuli.

Akizungumza jana wakati wa ibada ya shukrani jijini Dar es Salaam, Askofi Marekana alisema siku hizo sio za kuvaa mavazi mapya, kula, kunywa kucheza mziki na kujifurahisha kwani ni kinyume na bibilia.  

“Jambo la pili  tunawaomba Watanzania na kila  mahali na katika makanisa yetu watoe sadaka ya shukrani kwa Mungu, Mfalme Sulemani alipokuwa  na maombi ya  kuombea hekalu Mungu akajibu maombi yake na kumwongezea viti vingine sababu ya sadaka aliyoitoa, ukisoma kitabu cha Nyakati pili sura ya saba aya ya kwanza inasema ‘Mfalme Sulemani alipokwisha kuomba akatoa sadaka kwa Mungu ng’ombe 22,000. 

“Kumshukuru Mungu sio kujipongeza, sio kula, kunywa na kuvaa, ni kutoa sadaka ya mioyo na kutoa sadaka kwaajili ya kazi ya Mungu, watu watoe sadaka maalum ya shukurani kwa Mungu kila mtu kwa dini yake,”alisema Askofu Marekana.

Aliwataka Watanzania kutoa sadaka kwa kuwasaidia watu wasiokuwa na uwezo kwa kuwapatia mahitaji mbalimbali kama vifaa vya kujikinga na corona .

 “akini kingine ni kumshukuru Mungu kwa kuwasaidia wahitaji,  wapo waliopoteza  makazi kwasababu ya mafuriko, kuna jamii  wanaishi katika mazingira ya ukata zaidi. 

“Kuna wasioweza kununua vitakasa mikono, ndoo za kunawia mikono, mask (barakoa)  na wengine hata chakula hawaweze kununua, tuwasaidie hawa kwani hii ndio sadaka tunayoweza kutoa kwa Mungu,”alisema. 

Alisema kanisa la wasabato lilianzisha maombi ya siku 100 duniani kote tangu mwisho Machi mwaka huu na yatafikia kilele Julai 4. 

“Lakini sambamba na maombi yanayofanywa na kanisa, Mei  21 Rais Magufuli alitoa wito kwa Watanzania kuwa na siku tatu za maombi ya kumshukuru Mungu kwa kile ambacho Tanzania imefanyiwa na Mungu na katika taarifa yake alizungumza na kuonesha jinsi ambavyo maambukizi ya corona yamepungua. 

“Tunamshukuru Mungu kuwa tulikuwa na maombi siku za nyuma sisi kama kanisa la Wadventust Wasabato tumeitikia wito wa Rais kushiriki katika maombi Mei 22, 23 na 24,”alieleza. 

Askofu Marekana alitoa wito kwa  Watanzania wote kutimiza wajibu wao kila mtu kwa nafasi yake, kujitoa kufanya kazi, kuendelee kuchukua tahadhari  na kuondoa hofu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles