Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro
Askofu mteule wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac Amani amesema taifa linatakiwa kuhifadhi uhai wa watu wake na kulinda haki.
Aidha, amesema taifa linahitaji uhuru, haki na amani ambayo ni tunu inayopaswa kulindwa.
Askofu Amani ameyasema hayo leo wakati akiongoza ibada ya sherehe ya kuagwa kwake baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa miaka 10 kabla ya kuteuliwa Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha.
Ibada imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, waumini, mapadre kutoka Parokia zote la Jimbo Kuu la Moshi na viongozi mbalimbali wa serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa zamani wa Kilimanjaro, Meck Sadicq, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba na Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya.
“Amani inapaswa kulindwa kutokana na kwamba amani ndiyo mwanga wa ulimwengu, ili binadamu atoke kwenye utumwa anahitaji amani, haki na uhuru,” amesema.
Pamoja na mambo mengine, Askofu huyo amesema ili binadamu atoke kwenye utumwa wa kila aina anahitaji vitu hivyo vitatu.