LONDON, England
TIMU ya Arsenal bado haijashinda mechi yoyote ya ugenini kwenye Ligi Kuu England msimu huu, baada ya kupoteza mechi mbili na kupata sare mchezo mmoja.
Watford wanakuja kwa kasi Ligi Kuu msimu huu baada ya kupata pointi katika mechi ambazo walikuwa katika nafasi kubwa ya kufungwa. Walikuwa wameshakubali kipigo cha 2-0 dhidi ya West Brom, lakini waliamka kipindi cha pili na kupata sare ya 2-2.
Bao la kusawazisha lilifungwa na Richarlison zikiwa zimebakia sekunde chache, na mchezaji huyo kufunga tena wakishinda 2-1 dhidi ya Swansea wiki moja iliyopita.
Kwa ufupi Watford wameanza vema msimu na timu yao inaonekana kuwa tayari kwa vita ya kukwea juu kwenye msimamo wa ligi hiyo msimu huu.
Lakini bado Watford hawajashinda mechi msimu huu. Walipata sare dhidi ya Liverpool na Brighton, pia walichezea kichapo kizito mikononi mwa Manchester City.
Arsenal hatimaye waliweza kusimama tena baada ya kuanza vibaya msimu huu. Walipoteza mfululizo mechi dhidi ya Stoke City na Liverpool wiki tatu za mwanzo, lakini mambo yanaonekana kuwa mazuri kwao sasa baada ya kushinda mechi tatu na sare moja katika mechi nne. Bado hawajaruhusu bao tangu kipigo cha kudhalilisha cha 4-0 katika Anfield.
Hata hivyo, Arsenal bado hawajashinda mechi ya ugenini kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Wamepoteza mechi mbili na sare moja na hawajafunga katika kipindi hicho.
Watford waliifunga Arsenal 2-1 katika Uwanja wa Emirates mechi ya msimu uliopita na kukomesha mwendo wa vipigo saba mfululizo Ligi ya England.
Mechi tisa za mwisho baina ya timu hizo kwenye michuano yote kulikuwa na wastani wa zaidi ya magoli 2.5.
Arsenal wameshinda mechi zote 5 walizocheza na Watford na kufunga mabao yasiyopungua mawili kila mechi.
Hata hivyo, inatarajiwa kuwa mechi ya kuburudisha kila timu ikiwa inataka ushindi wa kwanza nyumbani na ugenini katika kampeni za msimu huu.
Timu zote zina kiwango kizuri cha kufunga mabao, kwa hiyo tunatarajia kuona mabao mengi, timu zote zitafunga.
Watford inaonekana kuwa timu iliyokamilika na uwezo wa kujibu mashambulizi mara moja wanapofungwa.
Arsenal wanayo nafasi kubwa ya kushinda mchezo huu, licha ya kuwa ugenini.