26.5 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Anko Lundenga, chukua ushauri huu

lundenga

WIKIENDI iliyopita Fainali za Miss Tanzania mwaka huu, zilifanyika jijini Mwanza kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994 (miaka 22 iliyopita) baada ya kufunguliwa na serikali wakati ule.

Mrembo Diana  Edward kutoka Kinondoni, ameondoka na taji hilo. Nilikuwepo katika Ukumbi wa Rocky City Mall, Ghana jijini humo na nilishuhudia shindano hilo, mwanzo mwisho.

Yapo mambo kadhaa ya kushauri, lakini kwa ujumla niseme kongole sana Hashim Lundenga ‘Anko’, Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa shindano hilo.

Kufunguliwa kwa mashindano hayo, baada ya kufungwa na Basata kwa miezi kadhaa, kumekuja na mambo mengi ya tofauti.

Kumbe inawezekana kabisa warembo wetu wakaonyesha ubunifu wao katika mavazi bila kuharibu maadili yetu. Ni Miss Tanzania ambayo kwa hakika unaweza kutazama na mama yako mzazi bila ukakasi wowote.

Warembo wameonekana kufundwa vizuri, wanajiamini na wenye ushindani mkubwa. Waliopata bahati ya kuingia Top 5 tumeshuhudia wakijieleza vizuri na kujiamini sana.

Bila shaka ndilo lengo hasa la shindano hili, ili kujenga Tanzania yenye watoto wa kike wenye kujiamini kama hawa tuliowashuhudia wikiendi iliyopita jijini Mwanza.

Lakini pia naona si vibaya ikiwa nitaeleza kasoro ndogondogo zilizojitokeza ambazo ikiwa waandaaji watazirekebisha miaka ijayo, tutakuwa na Miss Tanzania bora zaidi.

Ratiba ya kuanza kwa shughuli ilibanwa, hafla ilianza saa tano na nusu usiku wakati watu walianza kuingia tangu saa moja, jambo hilo halikuwa sawa kwa hakika.

Jambo jingine ni listi ya watoa burudani, staa pekee usiku ule alikuwa ni Christian Bella peke yake. Hilo ni jambo la kuzingatia sana. Angalau basi kuwe na wasanii au bendi kubwa tatu ili kukidhi haja ya mashabiki waliolipa viingilio vyao.

Bila shaka, ucheleweshwaji wa ratiba ni pamoja na kutokuwa na wasanii wa kutosha wa kutumbuiza. Naamini wangekuwepo, wangeanza kupagawisha tangu mapema kabla ya washiriki kupanda jukwaani.

Pia kulikuwa na tatizo la vyoo, hili lilikuwa tatizo kubwa kwani watu hawakutoshelezwa mahitaji yao kwa vyoo viwili kwa kila jinsia vilivyokuwepo viwanjani hapo, hali iliyosababisha wengine kujisaidia nje ya vyoo hivyo.

Lakini kamati inapaswa kuangalia pia zawadi, kwa shindano kongwe kama Miss Tanzania kutoa zawadi ya gari aina ya Toyota IST, nadhani kuna ukakasi kidogo.

Ni vyema mwaka ujao zawadi ziboreshwe. Niliona orodha ndefu ya wadhamini, naamini wanaweza kufanya kitu kizuri na kikubwa zaidi kama mkikaa nao mezani.

Zaidi niseme kuwa hii ni Miss Tanzania mpya, nzuri yenye maadili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles