26 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

‘Amani iliyopo haisababishwi na majeshi, ni uweza wa Mungu’

Christina Gauluhanga, Dar es Salaam

Askofu wa Pentekoste Parishi ya Tabata, John Shusho amesema amani iliyopo hivi sasa haisababishwi na majeshi na endapo ikikosekana hata uchumi unaweza kuyumba.

Akizungumza katika ibada ya shukrani ya ujenzi wa Kanisa la Pentekoste Mji Mpya Chanika jana Julai 28, Shusho amesema  amani iliyopo hivi sasa itadumishwa endapo kila mmoja atatambua umuhimu wa mwenzake.

Pamoja na mambo mengine amesema amani iliyopo inasababishwa na viongozi wa dini kutoa elimu pamoja na kuiombea nchi hivyo ni vyema wote wakashirikiana kuijenga na kuondoa vikwazo vya kushindwa kuabudu ikiwamo mikesha kwani kuabudu usiku ndiko kwenye baraka nyingi.

“Viongozi wa dini kila kukicha wamekuwa wakihubiri amani hivyo ni vyema wakaondolewa changamoto inayoanza kujitokeza hivi sasa ya kukosa uhuru wa kuabudu,” amesema.

Hata hivyo, amewataka wanasiasa na viongozi wa dini nchini kujenga utamaduni wa kuvumiliana ili kudumisha amani iliyopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles