Renatha Kipaka, Bukoba
Mwenyekiti wa Jumiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Murshidi Ngeze ameiomba Serikari kuwapa kibali cha kujijengea Gereji katika Halmashari zote kote nchini ili kuepukana changamoto wanayoipata kutoka (TEMESA) Wakala waufundi na umeme
Kauli hiyo ameitoa jana wakati akizungumza na Mtanzania Digital na chombo hiki ofisini kwake Bukoba vijijini.
Ngeze amesema sababu ya kuwaza Serikari kutoa kibari chakuwa kila Halmashari iwe na gereji yake ni kutokana na Temesa kushindwa kuwahudumia kwa wakati wateja wao pindi wanapo peleka magari yao kutengenezwa.
“Kunawakati tulilalamika katika vikao mbalimbali juu ya hiyo Temesa lakini hakuna mabadiliko yoteyote yale sasa tumeamua kutengenezwa magari yetu sehemu nyingine I’ll kuepuka usumbufu,” anasema Ngeze.
Anasema kuwa jambo jingineTemesa Wana bei kubwa katika matengezo yao mfano, Oil inauzwa 15,000 katika maduka mengine na Temesa ni Sh 25,000 na bei hiyo nileja leja.
“Sasa mimi ninajiuliza mfano firita bei ya rejareja ni Sh 45,000 na Temesa inauzwa shilingi 90,000 kitu ambacho kumekuwa kikwazo kikubwa katika halmashari,” anasema Ngeze.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa (Temesa) Kagera, Mhandisi Zephrine Banyona akijibu malalamiko hayo anasema kuwa katika Mkoa wa Kagera kwa upande wa halmashari ni Muleba tu ambayo inayaleta magari yake na nikayatengeneza.
Banyona anasema kuwa halmashari zingine zinamadeni sugu kwahiyo inakuwa changamoto hata katika utendaji wa kazi kati ya Temesa na hao wateja.
“Sababu inayoperekea magari kucherewa kutoka Temesa nimadeni halmashauri inaleta gari alafu kuripa inakuwa tatizo mpaka deni linakuwa Sugu mwisho inaonekana kama hatufanyi kazi kwa ufasaha,” anasema Kaimu Meneja huyo.
Mimi Temesa vifaa vya kutengeneza hayo magari navitoa kwa wazabuni sasa ninapochelewa kuwalipa nao hawezi kuendelea kunipa vifaa tena ili niendelee kutoa huduma.
Anasema kuwa bei ya oil nishiringi ya chini ni 12,000 na kulingana na muundo wa magari oil inafikia hadi Sh 30,000.
“Nitumie nafasi kusema kuwa wateja wetu wajitahidi kulipa madeni yao maana mpaka sasa deni tunalolidai Sh milioni 900,” amesema.