28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

AISHI NA MKASI TUMBONI KWA MIAKA 18

MATUKIO ya madaktari kusahau vifaa vya upasuaji kwenye miili ya wagonjwa si jambo geni duniani.

Ni matukio ambayo yameshuhudiwa mara kadhaa nchini Tanzania tena katika hospitali kubwa kabisa ya Taifa ya Muhimbili.

Lakini suala la vifaa hivyo kubakia mwilini mwa mgonjwa kwa miaka mingi bila kutambua kabla ya kuja kubainika karibu miongo miwili baadaye ni suala lingine.

Hilo limemtokea mwanamume mwenye umri wa miaka 54 nchini Vietnam, Man Van Nhat.

Mapema mwaka huu, Nhat aliondolewa mkasi wa upasuaji uliosahaulika wakati wa akifanyiwa operesheni tumboni mwake miaka 18 iliyopita.

Televisheni ya Taifa ya Vietnam (VTV) iliripoti kuwa Man Van Nhat, alilalamika maumivu ya tumbo yaliyobainisha tatizo hilo baada ya juhudi za kulikabili kwa dawa kutozaa matunda.

Kifaa hicho kilisahaulika wakati alipofanyiwa upasuaji wa dharura uliotokana na ajali ya barabarani mwaka 1998.

Kwa mara kadhaa Nnat alikuwa akihisi maumivu ya tumbo na alipokwenda hospitali alipewa dawa za kutuliza vidonda vya tumbo.

Lakini baada ya uchunguzi wa X-ray, ambao ulifanyika mwaka jana ikabainika kuwa chanzo cha maumivu yake hayo kuwa ni kifaa hicho.

Alifanyiwa upasuaji mwingine wa saa tatu kuondoa mkasi huo ambao ulionekana ukiwa na kutu.

Ukiwa na urefu wa sentimita 15 ulikuwa umegawanyika baada ya kumeguka na hivyo kusababisha maumivu hayo.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Back Kan, Trinh Thi Luong ameiambia VTV, kwamba maafisa wapo katika jitihada za kumsaka yule aliyekiacha kifaa hicho katika tumbo la Nhat.

Amesema hata kama tayari wamestaafu watawasaka ili iwe funzo kwa madaktari wengine. Ila hadi sasa wahusika wa uzembe kama si uhalifu wa makusudi bado hawajapatikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles