22.5 C
Dar es Salaam
Thursday, July 4, 2024

Contact us: [email protected]

ACT Wazalendo yapinga TAMISEMI kuandaa uchaguzi Serikali za Mitaa

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Chama cha ACT Wazalendo kimesema hakikubaliani na kitendo cha Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kufanya maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa inavunja sheria.

Hayo yamebainishwa leo Juni 12, 2024 na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu wakati akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.

Shaibu amesema Juni 11, 2024 wamepokea barua kutoka TAMISEMI ikiwaeleza kuwa wanaendelea na mchakato wa maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kuwaalika katika kikao cha kutoa maoni ya kanuni zitakazosimamia uchaguzi huo, kitakachofanyika Juni 15 mwaka huu, jijini Dodoma.

Ameeleza kuwa kitendo cha TAMISEMI kufanya maandalizi hayo ni kupoka mamlaka ya Tume Huru ya Uchaguzi, hivyo watahudhuria kikao hicho kwa lengo la kwenda kuitaka TAMISEMI isimamishe mchakato huo.

“Msimamo wetu sisi wa muda mrefu kama ACT Wazalendo ni kwamba uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi. Hatua yoyote inayochukuliwa na TAMISEMI kuhusu usimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni batili na kinyume cha sheria,” amesema Shaibu.

Aidha amesema chama hicho kimepanga kushirikiana na Asasi za Kiraia ili kufungua kesi ya kuzuia machakato wa maandalizi ya uchaguzi huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles