29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Ikulu yawagomea Ukawa

Baadhi ya viongozi wa Ukawa wakijadiliana jambo
Baadhi ya viongozi wa Ukawa wakijadiliana jambo

SHABANI MATUTU, DAR NA FREDY AZZAH, DODOMA

SIKU moja baada ya viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), kumtaka Rais Jakaya Kikwete kusitisha shughuli za Bunge Maalumu la Katiba, hatimaye Ikulu imeibuka na kusema haina mpango wa kulivunja.

Uamuzi huo wa Ikulu umetolewa jijini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipokuwa akizungumza na MTANZANIA.

Alisema Bunge Maalumu la Katiba lilianzishwa na linaendeshwa kwa mujibu wa sheria ambayo haina kifungu chochote kinachomtaka rais kulisitisha.

“Hakuna mpango huo kwa hivi sasa, Bunge Maalumu la Katiba limeanzishwa na linaendeshwa kwa mujibu wa sheria. Sheria hiyo haina kifungu cha rais kulisitisha,” alisema.

Sitta awashangaa

Akizungumzia kauli hiyo ya Ukawa, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta, alisema Bunge huendeshwa kwa mujibu wa sheria, na wanaosema lisitishwe hawana hoja kwani kila siku wamekuwa wakibadilika.

“Bunge hapa linaendesha shughuli zake kwa mujibu wa sheria, hawa watu kila siku wana hoja mpya,” alisema Sitta.

Alisema kuwa vitisho wanavyovitoa havimshtui.

“Kazi yao ni kulishambulia Bunge Maalumu tu, wanasema gharama, hata uchaguzi una gharama zake,” alisema.

Awali akizungumza na jumuiya ya wafugaji waliotembelea ofisini kwake mjini Dodoma na kuwasilisha mapendekezo wanayotaka yaingizwe kwenye Katiba mpya, Sitta alisema waliotoka nje ya Bunge hilo na sasa hivi wanapiga kelele wakitaka lisitishwe, hawawatakii Watanzania mema.

“Walioko hapa wanatosha kabisa kuendelea na mchakato mpaka mwisho,” alisema Sitta.

Juzi, Ukawa walitoa masharti manne kwa Rais Kikwete, ikiwamo kumtaka asitishe shughuli za Bunge Maalumu la Katiba ili wajumbe wake wasiendelee kufuja fedha za Watanzania.

Tamko hilo lililotolewa na wenyeviti wa vyama vya NCCR-Mageuzi, CUF na Chadema, vinavyounda umoja huo.

Hata hivyo, tamko lao halikumpa Kikwete siku ya mwisho ya kutekeleza agizo lao.

Mbali na hatua hiyo, pia wamemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi maalumu juu ya matumizi ya fedha za Bunge hilo, kuanzia Bunge la Bajeti lililopita, wakidai wamebaini kuwapo ufisadi na kukosekana maelezo sahihi.

- Advertisement -

Related Articles

5 COMMENTS

  1. UKIWA sijui ukawa sasa wanaanza kutapatapa. Wamekosa sapoti sasa wanaanza kutoa vitisho. kama ni mikutano ya hadhara nchi nzima mbona waliifanya na kushindwa kupata walichokitaka?

    HONGERA KIKWETE uzi ni ule ule tu usiwalegezee. Sasa umewabana kwenye angle ya nyuzi 90.

    Na hata hao wapiga filimbi wao wa kutoka kanisa katoloki sasa wameanza kuwachoka.

    • hapo kati ya ukawa na sita nani haitakii tanzania mema? watanzania wa sasa na wale wa zamani enzi za kina sita ni tofauti huwezi kuwadanganya tena!

      ukitakakujua ni uongo angalia mifugo ni suala la muungano? iweje leo waijadili kuingiza kwenye katiba? hizo ni siasa tu, suala la ardhi ni la muungano? uvuvi nishati na madini mbona sanaa za waazi wazi! kivuko kigamboni hakuna huyu anasema hivi na yule anasema hivi kutaka tu kuwahadaa wananchi sio tabia nzuri.

      duniani kote serikali kazi yake kubwa ni kuwafanya wananchi waifurahie nchi yao lakini hap TZ inakuwa kama adhabu!

  2. UKIWA sijui ukawa sasa wanaanza kutapatapa. Wamekosa sapoti sasa wanaanza kutoa vitisho. kama ni mikutano ya hadhara nchi nzima mbona waliifanya na kushindwa kupata walichokitaka?

    HONGERA KIKWETE uzi ni ule ule tu usiwalegezee. Sasa umewabana kwenye angle ya nyuzi 90.

    Na hata hao wapiga filimbi wao wa kutoka Kanisa Katoliki sasa wameanza kuwachoka.

  3. UKAWA rudini Bungeni lazima mjue kwamba Bunge la Katiba ndio chombo sahihi cha kisheria cha kuipitia Rasimu/draft ya Katiba, na rasimu au draft yoyote lazima ipitie kwenye chombo sahihi ambako itafanyiwa masahihisho/marekebisho kama lazima kabla ya kuthibitishwa.Ndio maana Bunge limepewa siku nyingine 70 LIsiwe “rubber stamp”.Kwa sasa kwa kweli mnaudhi wananchi wengi, badala ya kuwapa support.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles