25.5 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

Cannavaro afunguka kilichomsibu kustaafu

cannavaro gotiNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

BEKI na nahodha wa klabu ya soka ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amemjibu kocha mkuu wa timu ya soka ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa, kwamba hakuridhika na utaratibu alioutumia katika kumuondolea majukumu ya unahodha aliyokuwa nayo katika timu ya taifa.

Kauli ya Cannavaro imekuja baada ya kufanya uamuzi mgumu wa kustaafu, siku chache tangu Mkwasa kumtangaza mshambuliaji wa klabu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta, kuwa nahodha katika michuano ya kimataifa na Cannavaro nahodha kwa michuano ya Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani maarufu kama Chan.

Samatta alitangazwa nahodha mpya wa kikosi hicho siku chache baada ya kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, akichukua nafasi ya mkongwe huyo ambaye alikuwa nahodha wa kikosi hicho kwa muda wa miaka 10 tangu aliporithi kijiti hicho kutoka kwa Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’.

Akizungumzia hatua hiyo jana jijini Dar es Salaam, Cannavaro alisema hana kinyongo na Mkwassa wala mchezaji aliyepewa nafasi ya unahodha (Samatta), lakini hakuridhishwa na utaratibu uliotumika katika kutoa majukumu hayo.

“Sina kinyongo na Samatta kwa kuwa ni utaratibu wa kila timu duniani kufanya hivyo kutokana na mafanikio aliyoyapata mchezaji kimataifa, pia nina imani Samatta ataisaidia sana timu hii.

“Sijaridhishwa na utaratibu uliotumika kumpa cheo hicho Samatta kwakuwa ilitakiwa ifanyike kwa utaratibu ambao ungetoa fursa ya mimi kuagwa kama tulivyofanya kwa wengine wakati napewa cheo hiki,” alisema Cannavaro.

Cannavaro alisisitiza kwamba, hakupanga kustaafu mwaka huu kwa kuwa tayari mwaka jana alitangaza kufanya hivyo baada ya miaka miwili ijayo.

“Agosti mwaka jana nilisema kwamba ningestaafu baada ya miaka miwili ijayo, ghafla nilijikuta nimebadili uamuzi wangu kutokana na yaliyotokea,” alisema Cannavaro.

Beki huyo kisiki alieleza kwamba, asingependa kumuona beki mwenzake Aggrey Morris akistaafu wakati huu kwa kuwa bado ana msaada katika timu ya taifa.

“Nimesikia kupitia vyomba vya habari kwamba Morris anataka kustaafu, mimi ningemshauri asingefanya hivyo kwa kuwa bado ana muda mzuri wa kuisaidia timu ya Taifa,” alisema Cannavaro na kuongezea kwamba kwa sasa mawazo yake anayaelekeza katika kuisaidia klabu yake ya Yanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles