25 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Usalama waimarishwa kipindi cha kampeni

Na MWANDISHI WETU, MOSHI

MKUU wa Mkoa wa  Kilimanjaro Anna Mghwira amewataka Wanasiasa kutumia majukwaa yao ya kisiasa kutoa matamko ya matumaini kwa wananchi ili kuisadia nchi isonge mbele zaidi badala ya kutumia majukwaa hayo kutoa lugha za matusi.

Akizungumza na Amsha Amsha ya Uhuru FM 2020 nyumbani kwake alisema kipindi hiki kikitumiwa vizuri na wanasiasa kinasaidia kuwaweka wananchi pamoja lakini kikitumika vibaya kinaleta mfarakano na vurugu.

“Jukumu la wanasiasa kipindi hiki ni kuwaambia wananchi wataongeza thamani gani katika mambo yanayowagusa,maana vitu tayari vipo kinachotakiwa sasa ni kuboresha na kukarabati,” alisema.

Alisema dhamira ya serikali mkoa ni kuhakikisha Uchaguzi wa Oktoba 28 unafanyika kwa amani na utulivu na kusisitiza kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara  kuhakikisha amani inakuwepo kabla na baada ya uchaguzi.

Aliongeza kuwa hali ya usalama kwa sasa ni nzuri na hakuna vitisho vyovyote na kusisitiza kuwa wamejiandaa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu na kwamba hadi sasa hakuna vitisho vyovyote vya uvunjifu wa amani.

“Matamanio ya wanasiasa ya jukwaani yatafsirike kwenye maeneo watakayokuwa wanayaongoza, watambue kuwa hawaji kuongoza watu wapya bali ni watu wale wale waliokuwepo,” aliongeza.

Akizungumzia kuhusu mafanikio yaliyopatikana kwenye mkoa huo kupitia uongozi wa serikali ya awamu ya tano alisema kiasi cha Sh. Bilioni 40.3 kimetumika kwa ajili ya kugharamia elimu bila ya malipo mkoani humo.

Aidha alisema kiasi cha zaidi ya Sh. Bilioni 19 na sekondari zaidi ya Sh. Bilioni 43 kimetumika katika ukarabati wa miundombinu katika shule.

“Upande wa miundombinu ya barabara kiasi cha Sh. Bilioni 17 kimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa barabara,ujenzi wa hospitali mpya ya Rombo na Siha na Sh. Bilioni 12 kimetumika kukarabati pia jengo la mama na mtoto,” aliongeza.

Mkuu huyo wa mkoa alisema pia wanafuatilia viwanda ambavyo havijaendelezwa mkoani humo na kusisitiza kuwa mali za watanzania zitarudi kwa watanzania.

Akielezea upande wa sekta ya maji alisema kiasi cha Sh. Bilioni 18 zimetumika katika kuhakikisha wananchi wanapata maji.

“Upande wa mifugo na kilimo tuna mpango wa kuwachimbia visima wafugaji ili mifugo yao ipate maji,ukiangalia wilaya ya Mwanga ndio inaongoza kwak uwa na idadi kubwa ya wafugaji hivyo maji ni muhimu kwao,” alisema.

Wakati huo huo, Katibu wa CaCM, Jonathan Mabihya, amesema ushindi wa chama hicho kwa mkoa huo mwaka huu ni zaidi ya asilimia 99 kutokana na wananchi kuielewa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ilivyofanga maajabu makubwa kwa kipindi kifupi tu.

Akizungumza na Amsha Amsha ya Uhuru FM Mjini Moshi, katibu huyo wa CCM mkoa amesema Imani ya ushindi huo inatokana na utekelezaji mzuri  wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.

Kutokana na hali hiyo amewaomba wananchi kujitokeza katika mikutano ya kampeni ya CCM na hatimaye siku ya Jumatano ya tarehe 28 Oktoba kunipigia Kura za ndio CCM.

Miongoni mwa miradi inayoipaisha CCM katika ushindi wa mwaka huu amesema Ni Sera ya elimu bure, Afya kwa kuboresha na kukarabati Hospitali ya Mawenzi ya Mkoa wa Kilimanjaro, Miundombinu pamoja na mradi wa Maji ya Mwanga, Same na Korogwe ambayo wananchi wamekubali na kuipongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles