30.7 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maalim Seif, Hamad Rashid warejesha fomu urais Z’bar

Mwandishi wetu -Zanzibar

MGOMBEA urais wa Zanzibar, kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif Sharifu Hamadi, amerejesha fomu ya kuomba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imteue kuwania nafasi hiyo huku akiendelea kulia na kuenguliwa kwa wagombea wao.

Maalim Seif alirudisha fomu mbele ya Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Mstaafu, Hamid Mahmoud Hamid saa tano asubuhi jana.

Wakati akipokea fomu hiyo, Hamid  aliwaaomba wagombea kutojihusisha na rushuwa pamoja na suala la uhujumu uchumi kipindi chote cha uchaguzi.

Naye Maalim Seif alieleza kuwa anachosubiri ni uteuzi na baada ya hapo anawaomba wanachi wafike kwa wingi katika mikutano yake ya kampeni ambayo ataeleza sera zake.

Kuhusu  pingamizi, alisema yeye haogopi kwa sababu ni jambo la kisheria, lakini yasiwe ya kupikwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu wa chama hicho Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui, alidai kuna mpango wa kuhakikisha wagombea wao wa ubunge wanaenguliwa.

 “Wamepanga kuweka pingamizi katika majimbo yote 18 ya Pemba, lakini hasa katika majimbo ya Pandani, Gando, Chake Chake, Mkoani, Kiwani, Micheweni, na Ole,” alisema Mazrui.

Sambamba na majimbo hayo, Mazrui alidai kuwa pia CCM wamepanga kufanya hivyo katika majimbo nane ya Unguja ambayo wanahisi CCM hawawezi kushinda.

“Tunaitaka tume ya ZEC kuacha mara moja tendo hili ovu,” alieleza Mazrui.

Alieleza katika wakati huu CCM haisaidiliki kwani wananchi wameshaikataa na ushahidi ni katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

“Sisi hatuogopi pingamizi za kisheria, lakini sio upike kitu ambacho hakipo halafu utuondolee wagombea wetu, hatutokubali,” alisema Mazrui.

Kwa upande mwengine Mazrui aliitaka ZEC kujitathimini kwa kufanya makosa ya kutokuwepo kwa sehemu nzima ya tamko la uthibitisho wa wadhamini katika fomu ya uwakilishi.

“Mpaka tumepiga kalele sisi, tena kwa barua  ndio ZEC wametoa fomu hiyo, watawezaje kuwaondoa wagombea wetu kwa makosa ya kutengeneza?” alieleza Mazrui.

Kwa upande mwengine, mgombea wa ADC, Hamad Rashid Mohamed naye amerejesha fomu ya kugombea urais wa Zanzibar na kusema kipaumbele chake ni kuona wanafunzi wanasoma bure kuanzia msingi hadi sekondari.

“Wanafunzi wengine wanafeli kwa sababu ya kufikiria malipo, lakini Serikali yangu itaondoa hofu hiyo,” alisema Hamad.

Jana ilikuwa mwisho wa kurejesha fomu kwa wagombea wote Zanzibar na kuanzia Septemba kesho kampeni zinatarajiwa kuanza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles