29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Wahukumiwa maisha jela kwa kukutwa na bangi

Ramadhan Hassan -Dodoma

WATUHUMIWA Peter Kihando (32) na Ramadhani Bakari (28) wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kutokana na kukutwa na shehena ya bangi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alisema Kihando na Bakari walikamatwa na shehena ya bangi mwaka 2018 wilayani ya Bahi.

Alisema watuhumiwa walikuwa wameweka bangi hiyo sehemu ya mbele ya lori ikiwa kwenye magunia sita yaliyoshindiliwa katika mifuko maarufu kama ‘shangazi kaja’.

Alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisafirisha bangi hiyo kutoka Kahama kwenda Kibaha mkoani Pwani.

Alisema watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani na  kesi hiyo ilisimamiwa vizuri na washtakiwa kupatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.

Muroto alisema mafanikio ya kesi za uhalifu  zimesimamiwa vizuri na haki kutendeka na kupelekea watuhumiwa wa  kesi ya bangi kufungwa kifungo cha maisha.

Kamanda Muroto alisema pia wanamshikilia Hussein  Ibrahim(35)  mkazi wa  Kijiji cha Sejeli wilayani Kongwa kwa tuhuma za kukutwa na mabegi mawili ya bangi yenye ujazo wa kilogramu 35.

Alisema mtuhumiwa alikuwa akisafirisha katika basi la Simba Mtoto  linalofanya safari zake kutoka Dodoma kwenda Tanga.

Alisema mtuhumiwa amefikishwa mahakamani na kesi inaendelea kusimamiwa.

Pia alisema katika msako uliofanyika Julai 15 mwaka huu katika kijiji cha Kiboriani wilayani Mpwapwa walimkamata Joram Msigala (35) mkulima akiwa amelima bhangi katika shamba lake lenye ukubwa wa ekari 3.

Kamanda Muroto alisema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles