32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

PUMA ENERGY TANZANIA YANG’ARA TUZO  ZA MWAJIRI BORA TANZANIA 2019

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya.Mafuta ya Puma Tanzania ambayo ni namba moja katika biashara ya mafuta imeng’ara  kwa kujinyakulia tuzo nne katika hafla ya kuwazawadia waajiri bora nchini iliofanyika jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo ya utoaji tuzo iliandiliwa na Umoja wa Waajiri Tanzania (ATE) ambapo mgeni rasmi alikuwa  Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu anaeshughulikia Kazi, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemeavu Jenista Mhagama. 

Wakati wa kukabidhiwa tuzo hizo za ATE , Kampuni ya Puma Energy Tanzania ilitangazwa mshindi katika vipengele vifuatavyo.Tuzo hizo ni Mwajiri Bora mwenye mkakati bora zaidi wa kwa kuvutia na kutunza vipaji (Best Attraction and Retention Strategies), Mwajiri Bora katika kutunza na kusimamia wafanyakazi wenye umri mkubwa (Best employer In Managing Aged workface).

Pia kampuni ya Puma Energy iliibuka mshindi wa tatu katika kipengele cha Mwajiri bora kutoka sekta binafsi pamoja na kushika nafasi ya tatu katika tuzo kuu ya mwajiri bora wa mwaka 2019 baada ya TBL na GGM.

Akizungumza baada ya kushinda tuzo hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Dominic Dhanah aliwanpongeza washindi wote pamoja na makampuni mengine mbalimbali yalioshiriki katika tuzo hizo ma kwamba mwaka huu ameshuhudia mtanange mkali baina ya kampuni jambo linaloashirikia uboereshwaji mkubwa wa mazingira ya biashara nchini.

‘Lakini kubwa zaidi uboreshwaji wa sera za usimamizi wa rasilimali watu  nchini.Mwaka huu 2019 Puma Energy Tanzania imesani mkataba wa hali bora mahali pa kazi ( Collective Bargaining Agreement) na chama cha wafanyakazi TUICO, mkataba huu umeboresha Sanaa hali na mazingiira ya kazi kwa wafanyakazi wa kampuni yetu.

“Kama kampuni namba moja Tanzania katika biashara ya Mfuta ni wajibu wetu kuendelea kuboresha hali za wafanyakazi wetu lakini zaidi jamii mbalimbali zinazo tuzunguka. Tutaendelea kufanya wajibu wetu kama Mwajiri makini nchini Tanzania,”amesema Dhanah.

Kuhusu kampuni hiyo, Dhanah amesema kuwa Puma Energy Tanzania ni kampuni ya mafuta iliyosajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba  inamilikiwa kwa pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano (Kupitia Msajili wa Hazina, Wizara ya Fedha) pamoja na Puma Investments Limited.

Amefafanua kila moja ikiwa na umiliki wa hisa kwa asilimia 50. Kampuni ya Puma ni ya mkondo wa kati kimataifa katika masula ya mafuta na pia kampuni ya mafuta inayojihusisha na uhifadhi mkubwa na usambazaji. 

“Majukumu makuu ya kampuni ni masoko na usambazaji wa bidhaa za petroli ndani ya Tanzania. Kampuni inauwezo wa kuhifadhi jumla ya lita za mafuta  94 milion, vituo 52 vya mafuta maeneo mbalimbali nchini na inahudumia viwanja vinane vya ndege,amesema Dhanah. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles