25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

JPM ateta na ujumbe maalumu Ikulu

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amemhakikishia Rais Dk. John Magufuli kuwa matukio ya mashambulizi dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini sio msimamo wa Serikali ya nchi hiyo na kwamba Serikali hiyo itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa kidugu na kihistoria na Tanzania.

Ramaphosa amemtuma mjumbe maalumu, Jeffrey Radebe ambaye ni Waziri wa Nchi mstaafu wa Afrika Kusini, aliyeongozana na Mshauri wa Rais wa Afrika Kusini katika masuala ya ushirikiano wa kimataifa, Dk. Khulu Mbhatha, kuwasilisha barua yenye ujumbe huo kwa Rais Magufuli, jana Ikulu Dar es Salaam.

Katika ujumbe huo, Ramaphosa alifafanua kuwa Afrika Kusini inatambua mchango mkubwa wa Tanzania kwa nchi hiyo wakati wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi na kupigania uhuru ambapo ilijitolea kambi na misaada mbalimbali kwa wapigania uhuru.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli alisema Tanzania itaendelea kushirikiana na Afrika Kusini na amesisitiza ushirikiano zaidi katika maeneo ya biashara na uwekezaji.

Wakati huo huo, Rais Magufuli alikutana na Mjumbe Maalumu wa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, Hirut Zemene Kassa.

Katika ujumbe huo, Waziri Mkuu Ahmed amemuhakikishia Rais Magufuli kuwa Ethiopia itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles