25.8 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Harmonize kuongeza idadi ya wasanii bungeni?

SWAGGAZ RIPOTA

NYOTA ya msanii wa Bongo Fleva, Rajab Kahali ‘Harmonize’, imeendelea kung’aa mara baada ya wiki hii kuwa gumzo kufuatia kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kumtaka agombee ubunge katika jimbo la Tandahimba, Mtwara.

Mapema wiki hii huko Lindi, Harmonize alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza katika ziara ya Rais na katika pongezi zilizotolewa, Magufuli alichombeza kiu yake ya kutaka kumwona msanii huyo akigombea na kuwa mbunge.

Bosi huyo wa Konde Music Worldwide, amekubali kutii kauli hiyo na anaamini yeye pamoja na wananchi wa jimbo la Tandahimba wanaweza kuitekeleza sababu kauli ya Rais ni sheria.

Akimshukuru Rais Magufuli, Harmonize alisema:“Kauli yako tukufu ni sheria, nikiwa kama mwananchi wa kawaida sina budi kutii lakini pia wananchi wenzangu wa jimbo la Tandahimba wameipata kauli yako bila shaka kwa pamoja tunalifanyia kazi.”.

Kwa muktadha huo, endapo Harmonize akafanikiwa kuwa Mbunge basi atakuwa ameongeza idadi ya wasanii ambao ni viongozi katika ngazi ya ubunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Harmonize, ameendelea kupokea pongezi kutoka sehemu mbalimbali wakiwamo mashabiki zake wanaoishi nje ya Tanzania ambao wanafurahia kuona, Konde Boy ameaminiwa na Rais kwa kiwango kikubwa.

Licha ya kupata nafasi hiyo adimu ya kuaminiwa na Rais, miongoni mwa mashabiki zake wameingiwa na hofu na kuona kitendo cha staa huyo wa  wimbo, Kwangwaru kuingia kwenye siasa kitapunguza kasi ya kuwapa burudani.

Tunafahamu mbunge ana majukumu mengi ya kuwahudumia wananchi hivyo mbunge akiwa msanii anakuwa na majukumu mara mbili ya kuhudumia jimbo na kuwahudumia mashabiki wa muziki.

Ingawa tunaona Mbunge kama Joseph Haule ‘Profesa Jay’, ameweza kuliwakilisha vyema jimbo lake la Mikumi lakini pia katika muziki ameendelea kudondosha ngoma kali kama kawaida.

Je kama wana Tandahimba wakampa nafasi ya ubunge Harmonize, ataweza kuhudumia jimbo na kuwahudumia mashabiki zake kwenye muziki hasa hiki kipindi ambacho ametoka WCB na ameanza kujitegemea mwenyewe.

Kwakuwa kipindi hiki ni muhimu zaidi kwa  Harmonize ambaye anaijenga himaya yake ya Konde Music Worldwide, yenye lengo la kuwa tishio barani Afrika na bila shaka hilo ataliweza kama ataweka vizuri mipango yake.

Wakati Harmonize akiendelea kuwa gumzo katika suala hilo la ubunge. Clouds Media wamefungua milango upya kwa msanii huyo na kuanza kumpa sapoti tena ikiwa ni muda mfupi baada ya kuondoka WCB.

Inafahamika kuwa Clouds Media na WCB wapo kwenye matatizo ya kibiashara na hawapeani sapoti kwenye kazi zao lakini mapema jana, kurasa za mitandao ya kijamii za  Clous Media zilimwombea kura Harmonize katika tuzo za MTV EMA hivyo kuonyesha hawana tena bifu na Harmonize.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles