Amina Omari,Tanga
Halimashauri ya Jiji la Tanga imekabidhi vitambulisho 163 vya bima vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 4.8 kwa watoto wenye ulemavu chini ya umri wa miaka 18.
Akikabidhi vitambulisho hivyo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu na utaratibu wa Ukimwi, Stella Ikupa amesema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha inatoa fursa sawa kwa makundi yote yenye uhitaji nchini.
Amezitaka Halimashauri kuhakikisha zinapotenga bajeti ya kununua madawa katika hospitali zake kuwepo na bajeti ya mafuta maalum kwa watu wenye ulemavu ili nao waweze kupata huduma hiyo.
Awali Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kuwa vitambulisho hivyo vitawawezesha watoto wenye ulemavu kupata uhakika wa matibabu kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya Rufaa ya Bombo iliyoko mkoani humo.