28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ndege zisizotumia rubani kukagua uchafu Dar

MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Open Map Development Tanzania (OMDT) imezindua ndege zisizotumia rubani (drones) zitakazokuwa zinaangalia maeneo yaliyojificha yenye mkusanyiko wa uchafu unaozuia maji kutembea katika mitaro na kusababisha mafuriko na magonjwa ya milipuko wakati wa masika.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jana Dar es Salaam, msimamizi wa teknolojia hiyo, Fredrick Mbuya alisema ndege hiyo itakuwa inatumiwa na watu wanaofanya shughuli za kukusanya taka katika maeneo mbalimbali na kwamba imewekewa mfumo ambao unaweza kugundua eneo lenye uchafu hata kama limejificha.

“Tunajua tuna changamoto   kubwa ya kutambua uchafu uliopo katika  maeneo mbalimbali, hasa katika mito na sehemu zenye miti mingi, hizi taka zinapojaa katika maeneo hayo zinazuia maji kutembea katika mifereji na kusababisha mafuriko katika kipindi cha mvua,” alisema Mbuya.

Alisema mbali na kuonyesha takataka zilipo, teknolojia hiyo pia itakuwa inaonyesha eneo la kwenda kutupa takataka hizo na  umbali wake kutoka hapo zilipo.

Mbuya alisema mara nyingi watu wa mazingira wamekuwa wakiuwaza Mto Msimbazi pekee kwakuwa ndiyo njia kuu ya maji, kwamba unakuwa unahifadhi takataka nyingi zaidi, lakini yapo maeneo mengine kama Mto Mbezi na Mto Ng’ombe.

Alisema teknolojia hiyo itasaidia kuhakikisha Jiji la Dar es Salaam linakuwa safi pamoja na kuondoa mafuriko yanayosababishwa na kuziba kwa mifereji katika baadhi ya maeneo.

Kwa upande wake, mmiliki wa Kampuni ya Sharon Group of Company inayojihusisha na kuzoa takataka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam, Sawe Shiwaria, alisema wamekuwa na changamoto kubwa katika uzoaji wa takataka kwakuwa  mara nyingi wanakuwa na uwezo wa kuzikusanya katika maeneo ya wazi pekee.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles